• Skip to content
  • Jump to main navigation and login

Nav view search

Navigation

  • Mwanzo
  • ICC
  • ICTR
  • Ripoti kwa kila kesi
  • Rwanda
  • Ripoti nyingine
  • Tafuta
  • Kujiunga

Search

  • EN
  • FR
  • SW
  • RW
Vous êtes ici : Mwanzo

Radio News SW

Podcast Feed

TAARIFA ZA HIVI KARIBUNI

21.12.12 - MAJUMUISHO YA WIKI(AUDIO)

Arusha, Desemba 21,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) wiki hii imemwachia huru, kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mathieu Ngudjolo.Nayo Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), imehukumu kifungo cha miaka 35 jela, Waziri wa zamani wa Mipango, Augustin Ngirabatware baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya kimbari.Habari zaidi na Nicodemus Ikonko.

21.12.12 - MAJUMUISHO YA WIKI - ICC YAMWACHIA HURU KIONGOZI WA WANAMGAMBO,NGIRABATWARE KUTUMIKIA MIAKA 35 JELA

Arusha, Desemba 21,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) wiki hii imemwachia huru, kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mathieu Ngudjolo huku Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), ikimhukumu kifungo cha miaka 35 jela, Waziri wa zamani wa Mipango, Augustin Ngirabatware baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya kimbari.

20.12.12 – ICTR/NGIRABATWARE - WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA

Arusha, Desemba 20,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda(ICTR) imemhukumu kifungo cha mika 35 jela Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara baada ya kumtia hatiani kwa mashitaka matatu ya mauaji ya kimbari.

14.12.12 - MICT/CONVICTS - WAFUNGWA WAWILI WA ICTR WAACHIWA HURU MAPEMA

Arusha, Desemba 14,2012 (FH) – Taasisi ya Kimataifa inayorithi Kazi za Mahakama za Umoja wa Mataifa (MICT),Jumanne imewaachia huru kabla ya muda wao wa adhabu kuisha, watu wawili waliokuwa wanatumikia kifungo baada ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

14.12.12 - MAJUMUISHO YA WIKI - WAFUNGWA WAWILI WA ICTR WAACHIWA MAPEMA,MWENDESHA MASHITAKA WA ICC AOMBA MSAADA BARAZA LA USALAMA

Arusha, Desemba 14,2012 (FH) - Taasisi ya Kimataifa inayorithi Kazi za Mahakama za Umoja wa Mataifa (MICT),Jumanne imewaachia huru kabla ya muda wao wa adhabu kuisha, wafungwa wawili huku Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Fatou Bensouda alihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

14.12.12 - MAJUMUISHO YA WIKI(AUDIO)

Arusha, Desemba 14,2012 (FH) - Taasisi ya Kimataifa inayorithi Kazi za Mahakama za Umoja wa Mataifa (MICT),Jumanne imewaachia huru kabla ya muda wao wa adhabu kuisha, wafungwa wawili. Naye Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Fatou Bensouda alihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Habari zaidi na Nicodemus Ikonko.

07.12.12 - MAJUMUISHO YA WIKI (AUDIO)

Arusha, Desemba 07,2012 (FH) – Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wiki hii amewataka Wakenya kutowapigia kura wanasiasa wanaokabiliwa na kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).Nao maafisa waandamizi wa Taasisi Inayorithi Kazi za Mahakama za Kimataifa (MICT) wamesema juhudi za kuwasaka watuhumiwa vigogo watatu wa mauaji ya kimbari zinabakia kuwa kipaumbele cha taaisis hiyo.Habari zaidi na Nicodemus Ikonko.

07.12.12 - MAJUMUISHO YA WIKI - ANNAN AONYA WAKENYA KUTOWAPA KURA WATUHUMIWA,MSAKO WA VIGOGO WA MAUAJI YA KIMBARI HAUNA MWISHO

Arusha, Desemba 07,2012 (FH) – Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan wiki hii amewataka Wakenya kutowapigia kura wanasiasa wanaokabiliwa na kesi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), huku maafisa waandamizi wa Taasisi Inayorithi Kazi za Mahakama za Kimataifa (MICT) wamesema juhudi za kuwasaka watuhumiwa vigogo watatu wa mauaji ya kimbari zinabakia kuwa kipaumbele cha taaisis hiyo.

01.12.12 - ICTR/NGIRABATWARE - KESI YA MWISHO ICTR DHIDI YA WAZIRI WA ZAMANI KUTOLEWA HUKUMU DESEMBA 20

Arusha, Desemba 1,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda(ICTR) itatoa hukumu ya kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara Desemba 20, 2012, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo.

30.11.12 - MAJUMUISHO YA WIKI (AUDIO)

Arusha, Novemba 30, 2012 (FH) – Jarida moja la kila wiki la Ufaransa limechapisha habari kwamba polisi nchini Ujerumani walimkosa kumtia mbaroni mwaka 2007, mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda anayesakwa vikali, Felician Kabuga.Naye Mwendesha mashitaka nchini Norway ameiomba mahakama impatie kifungo cha miaka 21 jela mfanyabiashra mmoja wa Rwanda kwa kushiriki kwake katika mauaji ya kimbari mwaka 1994.Habari zaidi na Nicodemus Ikonko.

  • La Habari la Hirondelle
  • Marejeo
  • Muktadha wa jumla
  • Hirondelle ilivyo sasa
  • Kikundi
  • Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
  • Mazingira ya Vyombo vya Habari
  • TPIR
  • Katiba ya IDTA
  • Sehemu ya picha
feed-image RSS