Justice Info

Hirondelle Leo

Tokea ilipoanza mwaka 1996, Shirika la Hirondelle limeboresha aina tatu ya shughuli :
  • Maelezo
  • Uhifadhi wa nyaraka
  • Mafunzo
Tokea ilipoanza mwaka 1996, Shirika la Hirondelle limeboresha aina tatu ya shughuli: 

 Maelezo

 AIDF inatoa kwa raia wa Rwanda , Burundi , Tanzania, Uganda, DRC na Kenya pamoja na kwa jamii ya kimataifa shughuli taarifa zenye uhakika na haraka zinazohusu shughuli za mahakama ya ICTR na sheria ya Rwanda inayohusiana na mauaji ya kimbali. 

Utayarishaji
Ikiwa ni taarifa zinazoandikwa au zinazorushwa na kituo cha redio, AIDF inashughulikia moja kwa moja matukio yanayohusiana na kesi za mauaji yakimbali ya Rwanda katika ngazi tatu:
 

wandishi wa Habari wa Hirondelle1. Taarifa za kesi mbele ya mahakama ya ICTR zinatolewa kwa njia ya habari zinazotolewa na shirika
2.  Taarifa makini zinazoelezea kazi za mahakama ya ICTR
3. Mahojiano, maelezo ya kumtambua mtu, na redio ni vifaa muhimu katika kuifahamu mahakama ya ICTRAIDF inatayarisha ma mia ya taarifa na mashabaha kwa mwezi katika lugha nyingi.Shirika lina kituo chake cha redio kinachoiwezesha utayarishaji wa majarida na mashabaha kwa ajili ya redio za kitaifa na kimataifa.  

Usambazaji
Kazi ya uandishi ya shirika inatolewa kila siku na usambazaji wa electronika ya computa na kutabgazwa kwa njia ya mtandao( www.hirondelle.org) ambapo zaidi ya 450 ni wasomaji wa kudumu wakiwemo vyombo vya habari, mashirika pamoja na watu binafsi. Tovuti hiyo ni kama ofisi kurugenzi ambayo inahifadhi matangazo yote ya shirika katika orodha yenye kufuata utaratibu wa miaka na matukio wa kesi. 

Sambamba na hayo, idadi kubwa ya mashabaha wanaoripoti redioni wanalenga vituo vya redio vya kimataifa kama VOA na vinginevyo hasa vinavyorusha matangazo kwa Kiswahili na kinyarwanda. Pia wadau walijiendeleza na maredio kitaifa , kijamii na kibinafsi( Tanzania, Burundi…) Kutokana na vituo hivyo, taarifa zinazotayarishwa na shirika hazisikiki nchini Rwanda pekee bali katika eneo zima. 

Uhifadhi wa nyaraka

Likiwa mjini Arusha tokea uanzishwaji wa ICTR, AIDF imezitayarisha habari na taarifa zote na kuzalisha kinachoitwa leo kumbukumbu ya jamii yaani ‘ mémoire publique’. Makusanyo ya uzalishaji huo inapatikana katika mtandao wa shirika (www.hirondelle.org). AIDF pia inatoa marejeo ya bibliografia ya nchi za maziwa makuu. 
 

 Mafunzo

Kwanzia mwaka 1998, shirika liliwezesha mafunzo ya mara kwa mara kwa wandishi wa habari wa nchi za Afrika. Ripoti ya asili maalum ya ripoti kati ya sheria na vyombo vya habari vinahisi mafunzo muhimu ya wandishi wa habari vinayotumika katika nchi za maziwa makuu lakini katika nchi nyingi za Afrika. Mafunzo hayo yajibu mahitaji yenye manufaa ya kuweka adharani sheria ya kiafrika na kuchangia katika kuhamasisha haki za binadamu na kupiga vita uhuru wa kutoadhibiwa.