Justice Info

Idhini ya IDTA

Shirika la Habari, Hati na Uundaji (IDTA) la taasisi ya Hirondelle katika mahama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya Rwanda.

1. Kanuni muhimu za Taasisi ya Hirondelle:

AIDF ni kiungo cha taasisi ya Hirondelle yenye makao makuu nchini Geneva. Taasisi ya Hirondelle imeundwa kwa ajili ya kuunga mkono vyombo vya habari vinavyojitegemea katika maeneo yalioathirika na vita. Inaomba uhuru wa nguvu za kisiasa na kiuchumi, vile vile uhuru wa Mahakama ya ICTR na kesi inazozishughulikia. Inatetea taarifa isiyo na upendeleo. Hakuna mtu yeyote asiyeteuliwa na taasisi hiyo anayeweza kuzuia usambazaji wa taarifa zilizoshughulikiwa na kukamilishwa na vyombo vya habari vya Hirondelle.

2. Lengo la IDTA

Kwa kuzingatia umuhimu wa hukumu za mauaji ya kimbali au makosa ya jinai ulimwenguni kote zinazoamriwa na ICTR ili kuchangia  katika kupiga vita uathibishwaji , shirika la Hirondelle liliunda taasisi ya AIDF kwa ajili ya kutosheleza ipasavyo kazi zake. AIDF ni wakala wa vyombo vya habari inayopendekeza kwa vyombo vya habari vya nchi ya Rwanda, Burundi, Tanzania, Uganda RDC na Kenya pamoja na kwa vile vya kimataifa kupitia wananchi wake kushuhulikia matukio kwa uhakika, ukamilifu na kwa haraka   vikizangatia uwezo vilivyonavyo pamoja na kazi za ICTR.

Aidha, AIDF inasambaza kazi zake kwa kutumia mtandao yaani Internet ya taasisi ya Hirondelle. Katika hatua nyingine, AIDF inachangia katika shughuli za taaluma ya uandishi wa habari, na kazi za kisheria katika kwendeleza matumizi ya sheria kongwe.

3. Nyanja za matukio

AIDF inazipatia kipaumbele kazi za ICTR lakini pia inaweza kushughulikia matukio yote yanayohusika moja kwa moja na kesi za mauaji ya kimbali ya  Rwanda.

4. Aina ya matukio

AIDF inaripoti kwa usahihi, ukweli, na ukamilifu kupitia taarifa zinazotolewa na shirika na uhalisi wa ICTR. Inaweza pia kuripoti kwa kutumia muktadha wa uhalisi wa mahakama kwa kukumbushia matukio ya kihistoria au ya mahakama, kwa kutoa mhtasari wa wahusika muhinmu au kwa kueleweka zaidi, inaweka kando vipengele muhimu ili kusaidia uelewa halisi wa mahakama. Katiaka hatua hizo, taarifa zinatambulika wazi kwa kutaja vipengele kama "majumuisho", "makala", au "mhtasari" vinavyoendana na kichwa cha habari.

AIDF inaweza pia kutoa majarida na magazeti kupitia redio na taarifa za mahakama inazoshulikia.

5. Sawia

AIDF inaripoti katik ahali ya usawa mjadara wa ICTR. Haiwezi kuamua yenyewe kuripoti matukio ya kihistoria bali inaripoti matukio pekee ya mahakama . Usawa kati ya mtazamo tofauti wa pande zote mbili( Utetezi na Mashtaka) unasimia kwenye kuripoti kwa ujumla maelezo wakati wa mwendelezo wa kesi. Hakuna hata moja kati ya pande hizo inayotakiwa kujieleza nje ya mwendelezo wa kesi.

6. Matukio na maoni

AIDF inaweka utofauti mkubwa kati ya matukio na maoni. Inataja maoni endapo yatakuwa yameripotiwa. AIDF haibuni yenyewe haitoi uamuzi wa kijasiri au nyongeza yoyote.

7. Wajibu wa mdau

Mdau ana maelekezo maalum ambayo anatakiwa kuyarighisha kwa kuzingatia uhalisi maalum wa taarifa anazozifanyia kazi. Heshima kwa waathirika ni jambo analotakiwa kukumbuka na kuendeleza. Wakati wa jambo lolote nyeti, anatakiwa kuripoti kwa mkuu wake kwa kuzingatia mfumo wa  msonge wa madaraka uliyowekwa na taasisi ya Hirondelle.

8. Mamlaka ya sheria

Ombi lolote linalohitaji majibu litahakikiwa kwa kuzingatia sheria ya Uswisi. Kwa kila shughuli ya mahakama, mamlaka ziko nchini Gineva.