Justice Info

La Habari la Hirondelle

Shirika la Habari la Hirondelle linategemea na Taasisi ya Hirondelle, chama cha wandishi wa habari waliounda vyombo vya habari katika kanda hatari.

 

Mwaka 2006, shirika lilisambaza zaidi ya makala 1500 ya taarifa ya habari katika lugha ya kiingeleza, kifaransa, Kiswahili na kiniarwanda. Takribani makumi ya mashabaha au vituo vya redio kongwe viliwekwa kwenye tovuti au kusambazwa katika redio za taifa na za kimataifa.

 

Shirika linapenda kushirikiana na mwibuko wa jamii za kidemokrasia na stahimilivu na kuchangia katika kuleta maoni yanayowaajibisha raia na yaliyowazi kwa mazungumzo. Sheria imepewa kipaumbele kama mmoja ya masharti ya mapatano. Wanawake kwa wanaume wanaoishi katika kanda hatari wanahaki ya kupata habari inayofaa kuliko ushabiki.

 

Taasisi ya Hirondelle iliona siku mwaka 1995. Iliundwa rasmi mwaka 1996 ambapo ilianzisha vituo vya redio nchini Sudani, Liberia, Sierra Leone, Congo, na vile vile nchini Kossovo na Timor.

 

Napenda kuipongeza kazi inayofanywa na shirika la habari la Hirondelle kwani imetimza madhumuni ya kuinufaisha mahakama kwani ni nyongeza inayofaa na kuhitajika kwa kitengo cha habari cha mahakama. Tunaamini kwamba kazi ya Hirondelle itaendelea kwa kujitegemea. Ninaomba wafadhili wetu kuingilia kati mara moja pale ambapo shirika la Hirondelle litakua na upungufu kifedha.