Justice Info

Marejeo

Shirika la Habari la Hirondelle lipo mjini Arusha, nchini Tanzania, kwanzia mwaka 1996, limekua likishughulikia habari zinazohusiana na mauaji ya Rwanda ya 1994, hasa kuripoti kazi ya Mahakama ya Kimataifa Inayoshughulikia Kesi za Mauaji ya Rwanda (ICTR) pia na mahakama za Gacaca pamoja na kesi za kisheria nchini Rwanda.

TPIRKwanzia Decemba 2002, lilikuwa ni shirika pekee linaloshughulikia kesi hizo kwa kupitia habari za kila siku zikiripitiwa katika lugha ya Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili na Kinyarwanda.

Shirika pia linatoa offa kila mwaka kwa makumi ya wandishi wa habari wa kiafrika uwezo wa kujifunza kuhusu sheria ya kimataifa na uandishi wa vijarida vya mahakama.

Jina lake:
Lilibatizwa rasmi kwa jina la Shirika la Habari, hati na uundaji (AIDF), wengi wanaliita Hirondelle News Agency au Agence de Presse Hirondelle.

Jukumu lake:
-Kutoa habari inayojitegemea na yenye malengo kwa wanyarwanda  na watu wote ambao wanafurahia mwendelezo wa kesi zinahusu mauaji ya kimbali ya Rwanda.

-Kurahisisha upatikanaji wa hati zilizokamilika zinazohusu kesi za mahakama ya ICTR kwa jamii ya kimataifa.

-Kupanga mafunzo ya uwandishi wa habari za kisheria, sheria ya kimataifa, na haki za binadamu kwa wandishi wa habari wa kiafrika.

Walengwa:
-walengwa wakwanza kabisa wa AIDF ni wanyarwanda pamoja na raia wa Nchi za Maziwa Makuu. Shirika la Hirondelle linalenga pia kwa mapana wananchi wa kimataifa wakiemo wandishi wa habari, watafiti, wanafunzi wa vyuo vikuu, wanasheria , wanadiplomasia, nk. ambao wanahusika au wanavutiwa na swala la mauaji ya kimbali.

Lengo lake:

Shirika linalenga kuchangia katika kusambaza maoni ya kisheria na yenye amani katika Nchi za Maziwa Makuu pamoja na kushiriki katika kupiga vita kuathibiwa. Linamwelekeo wa kuunga mkono utaratibu wa mapatano ya kitaifa na kidemokrasia ya Rwanda. Kufikia malengo hayo, shirika linajitolea kutoa kwa vyombo vya sheria  vinavyohusika na mauaji ya Rwanda ushirikiano mkubwa hasa kwa walioathirika na mauaji hayo