Justice Info

Mauaji ya Kimbari ya Rwanda

MTIKISIKO ULIOTANGULIA MAUAJI

Arusha, Machi 26, 2004 (FH) - Yenye shughuli zisizo kawaida, yenye hofu, yenye mlipuko…watafiti wamekuwa wakichota mara nyingi katika rekodi ya aina hiyo kuelezea hali ya kisiasa iliyokuwepo nchini Rwanda kabla ya Aprili 6, 1994. Hivyo, hata kama kulikuwepo na uwingi wa viashirio vyo hofu vyenye ujumbe wa kificho wa Januari 1994 ambapo kamanda mtaalam wa mradi wa nguvu za umoja wa mataifa nchini humo Roméo Dallaire alionyesha uwezekano wa mauaji kwa kiwango cha juu, hakuna mtu aliyetarajia tukio la maafa. Akihojiwa baada ya tukio na gazeti la kila siku la "Le Temps", kuhusiana na swala hilo, katibu mkuu wa umoja wa mataifa ONU ambaye alikuwa msimamizi wa operesheni za kutunza amani duniani, Kofi Annan alijibu : " siku zote watu wanakuwa ashiki baada ya matukio".

Mwanzo kulikuwa na vita

Mwaka1959, wakati wa misukosuko ya kisiasa iliyofuatia upatikanaji wa uhuru nchini Rwanda, makumi ya maelfu ya wanyarwanda wa kabila la kitutsi walikimbilia nchi Uganda wakikimbia mauaji ya kikabila . ndani ya miaka 35, utawala ulichukuliwa na wahutu, kabila la wengi.
 octoba1, 1990, waasi wa kitutsi chini ya chama cha FPR, waliunda kikosi muhimu kwa ajili ya uzawa wa pili wa wanyarwanda waliokimbilia nchini Uagnda, na kuvamia utawala wa jenerali Habyarimana aliyekuwa kwenye utawala kwanzia mwaka 1973.

Wakihamanishwa nje ya nchi, huku upinzani ndani ya nchi ukikua, utawala ukagangamara. omaa, Menacé de l'extérieur alors que l'opposition intérieure grandit, le régime se durcit. Takribanwatutsi elfu kumi wa ndani ya nchi pamoja na wahutu waliokuwa wakidhaniwa kujumuika na waasi walikamatwa, baada ya uvamizi wa aibu uliofanyika Kigali usiku wa Octoba4 , 1990. Wakiwa wameachiwa huru, waliunda mbegu ya vyama vya siasa vya upinzani ambavyo vilikubalika mwaka 1991 mwaka mmoja baada ya mkutano wa France-Afrique uliofanyika La Baule, ambapo  François Mitterrand alisababisha msaada wa kiuchumi kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa. 

Matukio yenye lau moja

Mfumo wa vyama vingi umekuwa na misingi ya vita vya kiraia. Wakati wapiganaji wanabuni mbinu za kuboresha msimamo wao, vyama vya upinzani vilianza kupigania utawala. Habyarimana aliachia madaraka Aprili 1992 chini ya nguvu zenye mchanganyiko wa kusikitisha wa wafadhili.
Uwazi huo uliruhusu Kigali kuanza majadiliano ya moja kwa moja  mjini Arusha, Tanzania na waasi pamoja na chama chake cha siasa cha FPR. Majadiliano hayo yalichukuwa muda mrefu na mara kwa mara yalikuwa yakisitishwa na mwisho yakasimama kabisa kutokana na mauaji ya watutsi yaliyotokea Gisenyi kusini magharibi Decemba 1992 na Januari 1993. Mauaji hayo yalikuwa kama ukumbusho wa mauaji ya Bugesera, katika vijiji vya Kigali yaliyofanyika Machi 1992 au kwa wagogwe Gisenyi-Ruhengeri Januari 1991. Kufuatia mauaji hayo, FPR ilitoa hima ya adhabu Februari 1993 na kufika mlangoni Kigali baada ya kufanya mauaji mengi yaliyosababisha takriban watu milioni moja kukimbia. Vyama vya siasa viliendelea na mfumo huo nchini, sambamba na kutumia mara mbinu za kikatili. Tukio la aina yake litambulika katika kipindi hicho likiwa ni zoezi la kubohoza yaani kukomboa ambapo wanasiasa waliwapelekea vurugu viongozi wa serikali za mitaa kama magavana, mameya, ba madiwani waliogundulika kuwapinga. Ndipo lilipozaliwa wazo la kuunda « ailes jeunesse » yaani mabawa kwa vijana, kikundi ambacho kilichanganywa na jeshi la ulinzi. Mwaka 1994, Interahamwe wananchama wa kilichokuwa chama tawala, MRND, na Impuzamugambi wa chama kitendaji dhidi ya watutsi CDR, waligeuka kuwa mshale wa chuma wa mauaji ya kimbali. Katika kipindi hicho hicho, kulianzishwa redio ya wananchi iliyojulikana kama « Chombo cha Chuki ». Siku moja kabla ya mauaji ya kimbali, chuki dhidi ya watutsi ya kijarida cha Kangura na redio televisheni ya Mille collines, RTLM, vilifikia kiwango cha juu.  

Makubaliano baada ya mvutano

Ogasti 1993, mjini Arusha, makubaliano ya amani kati ya serikali na FPR yalifikia mwafaka baada ya mvutano usiowakawaida. Serikali ilifikiria uundaji wa kabineti yenye mtazamo mpana na kuwaingiza waasi wa FPR katika jeshi la nchi. Kwa ajili ya kuratibu makubaliano hayo, Umoja wa Mtaifa, ONU, ilituma kikosi cha wawakilishi cha watu 25000 kilichotambulika kwa jina la MINUAR. Mwanzo wa kazi ya kikosi hicho uliingiliana na kutolewa madarakani kwa rais wa Burundi Melchior Melchior Ndadaye aliyechaguliwa kidemokrasia na kuuawa kikatili Octoba 21, 1993. Tukio hilo lileta msukumo wa kuemdelea na mipango yao waasi wa FPR kama anavyosema mwanahistoria na mtendaji wa maswala ya haki za binadamu Alison Des Forges
Tukio hilo lilichimbuliwa na RTLM ambayo ilianza kutangaza baada ya miezi mitatu. Redio hiyo ilikuwa inarusha hewani nyimbo za kivita zilizokuwa zimekataliwa tokea makubaliano ya amani ya Arusha.

"Hutu power" Hutu Power

Katika hatua nyingine, Frodouald Karamira, tajiri mfanyabiashara, na mwanakamati ya uongozi ya chama cha MDR, chama kikubwa kati ya vyama vya upinzani, aliandaa mkutano wa kisiasa ambapo alitoa wito wa nguvu za kihutu kama Hutu ‘Power ‘ inayotafsiri uchungu wa kikabila wa wanachama wa vikundi vya siasa. Baadhi ya vikundi vya siasa vilijigawanya vikilenga ukabila na kugombea haki. Swala hili lilichelewesha kuweka serikali na bunge vya mseto kama ilivyokuwa inatarajiwa na makubalinao ya amani, vyama vingi viwasilisha orodha mbili. Januari5 ,1994, Habyarimana aliapishwa na kuwa rais wa nchi kwa kuzingatia makubaliano ya Arusha. Lakini hata hivyo, maelewano kati ya serikali na bunge hayakuwepo, kutokana na vikwazo vya kisiasa vilivyokuwa vikiendelea upande wa utawala na FPR. Hali ilizidi kuwa mbaya Februri21, alipouawa kiongozi na kivutio cha upinzani, waziri wa kazi za kijamii  Félicien Gatabazi ambaye aliuawa mbele ya nyumbani kwake. Kesho yake, kama ishara ya kulipiza kisasi, rais wa chama cha CDR, Martin Bucyana alipigwa na kundi lenye hasira kali Butare kusini, alikozaliwa Gatabazi. Mashambulizi mapya yalianza hasa Kigali na Cyangugu kusini magharibi, kwa ada ya Bucyana. Vita ya kiraia na muundo wa jeshi vilipamba moto, propaganda dhidi ya watutsi katika baadhi ya vyombo vya habari na virutubisho vilikusanywa kwa ajili ya kwanzisha maafa. Aprili6, 1994, saa mbili karibia na nusu za jioni, ndege iliyombeba rais Habyarimana ilisambalatika wakati alipokuwa anakaribia uwanja wa ndege wa Kigali. Baada ya masaa kadhaa, mauaji ya kimbali ya Rwanda yakaanza  

SIKU 100 ZA HOFU KUBWA : MTIRIRIKO WA MATUKIO YA MAUAJI YA HALAIKI YA RWANDA MWAKA 1994

Na Shirika la Habari la Hirondelle-Arusha

Aprili 6, 1994,saa 12.25 jioni- Ndege ndogo aina ya Falcon 50 iliyokuwa inatokea nchini Tanzania ililipuliwa angani wakati ilipokuwa inakaribia kutua katika uwanja wa ndege wa Kigali. Ndani ya ndege hiyo kulikuwemo Rais wa Rwanda Juvenal Habyarimana na Rais mwenzake wa nchi jirani ya Burundi, Cyprien Ntaryamira na wasaidizi mbalimbali wa marais hao ambao kwa pamoja walikuwa wanarejea nyumbani baada ya kushiriki kikao cha kidogo cha kanda kilichohusiana na utekelezaji wa Mkataba wa amani wa Arusha.

Saa chache baadaye, askari wa kikosi cha walinzi wa Rais, vikosi vya makomandoo na upelelezi pamoja na wanamgambo wa Interehamwe waliweka vizuizi vya barabarani kuzunguka jiji la Kigali. Taarifa za mauaji ya kisiasa zikaanza kupatikana.

Aprili 7- Waziri Mkuu, Agathe Uwilingiyimana, Rais wa Mahakama ya Katiba, Joseph Kavaruganda na mawaziri kadhaa wa serikali toka upande wa vyama vya upinzani waliuawa. Msako wa nyumba hadi nyumba na mauaji dhidi ya Watutsi yalianza.

Askari 10 wa Kibelgiji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Rwanda (UNAMIR) waliokuwa wapambe wa Waziri Mkuu nao waliouawa.

Askari wa serikali pia walianza kuua wagonjwa katika hospitali Kuu ya mjini Kigali (CHK).

Askari wa Kikosi cha Waasi cha Rwandese Patriotic Front (RPF) waliokuwa na makao yao makuu katika jingo la Bunge la Taifa (CND) walijitokeza mitaani. Mapambano makali yalizuka kati yao na askari wa kikosi cha walinzi wa rais.

Aprili 8- Mauaji yalisambaa katika maeneo mengine nchini. Watumishi wengi wa serikali wakiwemo mawaziri walikimbilia Ubalozi wa Ufaransa kupata hifadhi ya usalama wa maisha yao.Mamia ya watu waliuawa katika Chuo cha Mtakatifu Adrea kilichopo eneo la Nyamirambo, mjini Kigali.Mikutano mbalimbali iliendeshwa chini ya usimamizi wa Mkurugenzi katika Wizara ya Ulinzi, Kanali Theoneste Bagosora ili kuziba pengo la kikatiba lililojitokeza kufuatia kifo cha Rais. Baadhi ya maafisa ndani ya jeshi walikataa wazo la kutwaa madaraka kijeshi na badala yake waliamua kuunda serikali mpya.Aprili 9- Serikali ya mpito iliundwa kwa kumchagua Theodore Sindikubwabo kuwa Rais na Jean Kambanda kuwa Waziri Mkuu. Serikali hiyo iliundwa na mawaziri kutoka chama tawala wakati huo cha MRND peke yake na wajumbe toka vyama vya upinzani vilivyokuwa na msimamo mkali.Majeshi ya Ufaransa chini ya operesheni iliyojulikana kama Opereshini Amaryllis na askari wa Ubelgiji chini ya operesheni Silverback walianza harakati za kuwahamisha raia wa kigeni kuondoka nchini Rwanda. Familia ya Rais Habyarimana ilikuwa ya kwanza kuhamishwa na kupelekwa mjini Bangui, Jamhuri ya Afrika ya Kati na baadaye ikapelekwa Ufaransa.Aprili 12- Serikali ya mpito ilikimbia jiji la Kigali na kuweka makao yake makuu mjini Murambi mkoa wa Gitarama uliopo katikati ya Rwanda.Aprili 13- Ubelgiji iliamua kuvitoa vikosi vyake nchini Rwanda na kuwaacha maelfu ya watu waliokuwa wamekimbilia katika makao makuu ya vikosi hivyo ndani ya Chuo cha Kijeshi (ETO) bila ulinzi. Askari wa serikali na Interahamwe walishambulia chuo hicho. Maelfu waliuawa akiwemo Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Boniface Ngulinzira. Mauaji hayo yaliwasha moto wa kwanza wa mashambulizi ya askari wa serikali na wanamgambo wa Interahamwe dhidi ya maeneo yaliyohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi wa Kitutsi.Aprili 14- Mauaji makubwa yalifanyika hospitali ya Kibeho mkoani GikongoroAprili 15- Mauaji zaidi yalifanyika Nyarubuye mkoani Kibungo na mengine katika Parokia ya Mubuga mkoa wa Kibuye.Aprili 16- Mauaji makubwa yalifanyika katika Parokia ya Mugonero mkoani Kibuye.Aprili 18- Watutsi waliokimbilia kupata hifadhi ya maisha yao katika uwanja wa michezo wa Gatwaro mkoani Cyangugu walishambuliwa na maelfu kuuawa.Aprili 20-22- Askari na wanamgambo wa Interahamwe waliwashambuli wagonjwa katika hospitali ya chuo Kikuu cha Butare.Aprili 21- Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Rwanda (UNAMIR) kilipunguza idadi ya askari wake kutoka 5,500 hadi 270.Aprili 27- Baba Mtakatifu John Paul wa II amekuwa wa kwanza kutamka rasmi kwamba mauaji ya Rwanda ni “mauaji ya halaiki”.Aprili 28- Marekani imesita kutoa ufafanuzi kwamba mauaji ya Rwanda ni “mauaji ya halaiki”.Msema wa Ikulu ya Marekani, Christine Shelley amesema”…matumizi ya maneno ‘mauaji ya halaiki’ yana maana maalum katika medani ya sheria ingawaje haimaanishi kwamba yanahusu tu maamuzi ya kisheria. Kuna vingele vingine pia vinavyohusiha suala hilo.Aprili 30- Maafa makubwa ya kwanza kwa binadamu yametokea: Zaidi ya wakimbizi 250,000 walivuka mpaka kuingia nchini Tanzania katika siku moja kutokana na ushindi waliokuwa wanaendelea kupata Kikosi cha Waasi cha RPF.Mei 12- Kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupigania Haki za Binadamu hatimaye alitangaza rasmi kwamba maneno ‘mauaji ya halaiki’ yatumike kuelezea mauaji yaliyotokea nchini Rwanda.Mei 13-14- Kilima cha Muyira kilichoko katika eneo la Bisesero mkoani Kibuye ambacho kilikuwa ni miongoni mwa ngome kuu za mwisho za wakimbizi wa Kitutsi hakikuweza tena kuhimili mashambulizi. Vikosi vya pamoja vya askari, wanamgambo na raia walifanya mashambulizi makubwa dhidi ya wakimbizi hao na maelfu waliuawa.Katikatika ya Mei- Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lilikadiria kwamba watu walioteketezwa katika mauaji ya halaiki ya Rwanda walikuwa 500,000.Mei 22- Kikosi cha Waasi cha RPF kilifanikiwa kuukamata uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kanombe mjini Kigali.Mei 27- Mpango kabambe wa kwanza wa “kubadilishana wakimbizi” uliandaliwa na UNAMIR. Mamia ya wakimbizi wa Kitutsi na Wahutu waliokuwa wanaipinga serikali walioshikiliwa katika hoteli ya Mille Colloines walipelekwa katika eneo lililokuwa linadhibitiwa na RPF ambapo Wahutu waliokwama nyuma ya eneo la Remera lilikuwa chini ya RPF walipelekwa upande uliokuwa unadhibitiwa na majeshi ya serikali. Mabadilishano hayo yalifanyika katika eneo huru la mzunguko wa Kacyiru lisilomilikiwa na upande wowote wa mapambano.Mei 29- Serikali iliendelea kukimbilia upande wa Kaskazini zaidi na kuweka kambi mkoani Gisenyi, karibu na mpaka wa Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC-).Juni 2- Mji wa Gitarama ulitekwa na waasi. Siku tatu baadaye, viongozi 12 wa dini wakiwemo maaskofu watatu wa Kihutu waliokuwa wamebaki katika mji huo kuwalinda wakimbizi wa Kitutsi waliuawa na askari wa RPF.Juni 16- Waasi wa RPF walifanya shambulizi la kikomandoo nyuma ya maadui zao kuwaokoa wakimbizi waliokuwa wanapata hifadhi katika kanisa la Mtakatifu Paul mjini Kigali. Mamia ya wakimbizi waliokolewa na kupelekwa upande wa vikosi vya RPF.Juni 17- Wakimbizi waliuawa katika kanisa la Familia Takatifu kulipiza kisasa shambulio la kikomandoo lililofanywa katika kanisa la Mtakatifu Paul.Juni 22- Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha mpango wa Ufaransa wa kupeleka majeshi yake nchini Rwanda ili kuandaa eneo la kutolea misaada ya kibinadamu chini ya operesheni iliyojulikana kama “Turquoise.”Juni 28- Umoja wa Mataifa ulichapisha ripoti ya mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi.Julai 4 - Miji ya Kigali na Butare iliangukia katika udhibiti wa RPF na Ufaransa ilitangaza miji ya Kibuye, Gikongoro na Cyangugu kuwa ni maeneo huru kwa ajili ya huduma za kibinadamu.Julai 13 - Wakimbizi walianza kumiminikia mjini Goma (DRC) kwa mamia na maelfu.Julai 15 - Marekani ilisitisha rasmi kuitambua serikali ya zamani ya Rwanda.Julai 17 - RPF iliteka miji ya Gisenyi na Ruhengeri na kutangaza mwisho wa vita.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Maafa ya Rwanda mjini Goma (DRC) iliripoti kuwa zaidi wa Wanyarwanda milioni moja wamevuka mpaka kuingia nchini DRC.Julai 19 - Serikali mpya ya umoja wa kitaifa iliapishwa ambapo Pasteur Bizimungu alikuwa Rais, Meja Jenerali Paul Kagame, Makamamu wa Rais na Faustin Twagiramungu akawa Waziri Mkuu.