Justice Info

Muktadha wa jumla:

Mauaji ya kimbali ya Rwanda ya mwaka 1994 yalisababisha vifo vya watutsi pamoja na wahutu wasiokua na msimamo wa kikabila milioni moja katik asiku mia moja tu.

mafuvu ya walio kufa kwa mauaji ya kimbari Timu ya wanahabari kutoka Uswisi walioshuhudia matukio ya mauaji hayo, walianzisha kituo cha redio cha Agatasha  chenye malengo ya kuwasaidia wananchi kwa kusambaza habari ya kujitegemea katika lugha zifikazo tano.

Ndani ya miezi sita kati ya Agosti 1994 na Octoba 1996, redio hiyo ilitangaza bila kukoma, wasikilizaji walikadiliwa kati ya milioni nne na kati yao milioni moja walikua wakimbizi na waliohamisha makazi yao. Wasikilizaji hao ni raia wa Rwanda, Zaire( Congo), na Burundi.

Kutokana na mafanikio ya mradi huo, ilizaliwa Taasisi ya Hirondelle ikiwa na madhumuni ya kutoa habari inayokidhi mahitaji ya walengwa, isiokuwa na ubaguzi, na tulivu kwa wananchi ambao walikua hawana uwezo wa kuzipata kutokana na hali ya migogoro au matatizo asilia.

Mwaka 1994, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ilianzisha Mahakama ya kushughulikia kesi za Mauaji ya Rwanda (ICTR) yenye majukumu ya kuwatafuta na kuwaleta mbele ya sheria kisha kuwahukumu wanaohisiwa kuhusika na uvunjakaji wa haki za kimataifa za binadamu nchini Rwanda na katika nchi jirani.

{mosimage}Tokea ufunguzi wa ICTR, redio Agatashya ilipanua shughuli zake kwa kuhakikisha kuzifanyia kazi kesi za mahakama ya ICTR ambayo makao makuu yako mkoani Arusha nchini Tanzania. Hivyo jiwe la msingi la shirika la AIDF likasimikwa.

Kwa upande wa Taasisi ya Hirondelle (Fondation Hirondelle), mahakama hiyo, kutokana na mwenendo na mfano wake wa kipekee imeombwa kuwajibika kwa tahadhari na uaminifu kwa kutaja uasi unaoadhibishwa kama inavyosema haki ya kimataifa ya binadamu.

Pia Taasisi hiyo inaikadilia mahakama kuwa zaidi na jukumu la kuelimisha kuliko kuwaruhusu wananchi kuelewa yaliyotokea na kutupilia mbali kumbukumbu ya janga hilo la kusikitisha.

Tokea mwaka 2001, serikali ya Rwanda iliifufua Taasisi ya zamani inayojulikana kwa jina la « gacaca » ili kuweza kuharakisha hukumu ya washtakiwa  wapatao 120,000 walioko katika mahabusu ya nchini humo kwanzia kipindi cha mauaji ya kimbali. Utaratibu huo wa kimila unatumia utaalamu wa jamii ya wanyarwanda kabla ya ukoloni wenye msingi wa sheria shiriki na yenye ukaribu. Mahakama za gacaca zinahusisha zaidi ya majaji 250,000 katika kesi takribani 10,000 nchi nzima. Utendaji wa kesi za gacaca unalenga uwezekano wa mapatano ya kitaifa.

Kwa maana hiyo, shirika la Hirondelle imejiwekea malengo ya kufuatilia na kutangaza ndani ya muda mwafaka mwendelezo wa kazi za sheria inayotambulika kwa kiwango cha juu, nchini Rwanda na kesi zinazoshughulikiwa na gacaca. Tokea mwaka 2003, mwandishi wa habari wa shirika hilo anaishi Kigali.