Justice Info

Reports by trial

20.12.12 – ICTR/NGIRABATWARE - WAZIRI WA ZAMANI WA MIPANGO WA RWANDA AHUKUMIWA MIAKA 35 JELA

Arusha, Desemba 20,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda(ICTR) imemhukumu kifungo cha mika 35 jela Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara baada ya kumtia hatiani kwa mashitaka matatu ya mauaji ya kimbari.

01.12.12 - ICTR/NGIRABATWARE - KESI YA MWISHO ICTR DHIDI YA WAZIRI WA ZAMANI KUTOLEWA HUKUMU DESEMBA 20

Arusha, Desemba 1,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda(ICTR) itatoa hukumu ya kesi inayomkabili Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda,Augustin Ngirabatwara Desemba 20, 2012, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mahakama hiyo.

09.10.12 - ICTR/GATETE - APUNGUZIWA ADHABU TOKA KIFUNGO CHA MAISHA HADI MIAKA 40 JELA

Arusha, Oktoba 09, 2012 (FH) – Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumanne imempunguzia adhabu ya kifungo cha maisha jela hadi miaka 40,afisa mwandamizi wa zamani wa serikali ya Rwanda, Jean-Baptiste Gatete kwa kuhusika kwake na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini mwake.

19.09.12 - ICTR/NIYITEGEKA - ASHAURI ICTR IKATAE MAOMBI YA WAZIRI ALIYEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA

Arusha, Septemba 19, 2012 (FH) – Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR),ameiomba mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya Waziri wa zamani wa Habari wa Rwanda na mfungwa wa mauaji ya kimbari, Eliezer Niyitegeka, anayetaka kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya madai ya mashahidi kutoa ushahidi wa uongo katika kesi yake. ‘’Niyitegeka hajatoa kitu chochote kipya cha kuonyesha kuwepo kwa ushahidi wa uongo. Juhudi zake za kujaribu kwa mara nyingine kupinga matokeo yaliyobainishwa dhidi yake hapo awali hazina budi kutupiliwa mbali,’’ anaeleza James Arguin, Mkuu wa Kitengo cha Rufaa na Ushauri wa Kisheria, katika ofisi ya Mwendesha Mashitaka anaeleza katika hati ya kujibu maombi ya mfungwa huyo Jumatatu. Waziri huyo wa zamani ambaye hivi sasa anatumikia kifungo cha maisha jela nchini Mali, alitiwa hatiani na mahakama ya awali Mei 23, 2003 kwa tuhuma za mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu. Mahakama ya Rufaa nayo ilithibitisha hukumu na adhabu aliyopewa Julai 9, 2004. Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa imeshayakataa maombi matano kutoka kwa mfungwa huyo yaliyotaka mahakama ifanye marejeo ya hukumu yake. Katika maombi yake, Niyitegeka anataka Mahakama imwamuru Msajili wa Mahakama hiyo, imteue rafiki wa mahakama, kuchunguza ushahidi wa mashahidi wa mwendesha mashitaka hususan ni shahidi mwenye jina bandia la GGV, kwa lengo la kutaka hatimaye ashitakiwe kwa kutoa ushahidi wa uongo. Kama ombi hilo la awali halitakubalika mfungwa huyo anaomba afikiriwe ombi lingine la kuondoa amri inayomlinda shahidi huyo kutotoa ushahidi wake hadharani kwa kutumia jina bandia ili asitambulike kwa sababu za kiusalama ili sasa atambulike hadharani na kisha ashitakiwe mbele ya mahakama nyingine. Maombi ya Niyitegeka ya kuunda jopo la kusikiliza madai yake yalikubaliwa Septemba 7, 2012 na tayari yamepangiwa jopo la majaji watatu kuyasikiliza akiwemo Rais wa ICTR. NI/FK © Hirondelle News Agency

11.09.12 - ICTR/GATETE - HUKUMU YA KESI YA RUFAA YA GATETE KUTOLEWA OKTOBA 9

Arusha, Septemba 11, 2012 (FH) – Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Oktoba 9, 2012 itatoa hukumu ya kesi ya rufaa ya afisa mwandamizi wa zamani wa serikali ya Rwanda, Jean-Baptiste Gatete, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mahakama hiyo.

31.07.12 - ICTR/KESI - MAHAKAMA YA RUFAA YA ICTR KUTOA HUKUMU OKTOBA

Arusha, Julai 31, 2012 (FH) – Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) inatarajia kuwa na vikao viwili kabla ya mwisho wa mwaka huu kikiwemo kimoja cha kutoa hukumu, chanzo cha habari cha uhakika kililiambia Shirika la Habari la Hirondelle Jumatatu.

23.07.12 - ICTR/MILITARY II - MUINGEREZA KUONGEZA NGUVU TIMU YA UTETEZI KESI YA RUFAA YA SAGAHUTU

Arusha, Julai 23, 2012(FH) – Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imemruhusu mshauri wa masuala ya sheria wa Uingereza, Wayne Jordish kuongeza nguvu katika timu ya utetezi wakati wa kusikiliza rufaa ya afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda, Kapteni Innocent Sagahutu.

19.07.12 - ICTR/ACQUITTED - ICTR YAKATAA MAOMBI YA JOPO LA KUSIKILIZA KILIO CHA WALIOACHIWA HURU

Arusha, Julai 19,2012 (FH) – Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumanne alikataa maombi ya watu wanne walioachiwa huru kutaka aunde jopo litakalosikiliza madai yao kuhusu kukosekana kwa nchi za kuwapokea kwenda kuishi.

17.07.12 - ICTR/ACQUITTED - WALIOACHIWA HURU WATAKA ICTR IWASIKILIZE KUPATA KWA KWENDA KUISHI

Arusha, Julai 17,2012 (FH) – Watu wanne kati ya watano walioachiwa huru na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wamemwomba Rais wa Mahakama hiyo kuunda jopo litakalosikiliza madai yao kuhusu kukosekana kwa nchi ya kuwapokea.

21.06.12 - ICTR/ZIGIRANYIRAZO - ICTR YAKATAA MAOMBI YA ZIGIRANYIRAZO KUFIDIWA DOLA MILIONI MOJA

Arusha, Juni 21, 2012 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imeyatupa maombi ya Protais Zigiranyirazo aliyeachiwa huru na mahakama hiyo kutaka alipwe fidia ya dola milioni moja kwa madai ya kukiukwa kwa haki zake za msingi. Hata hivyo uamuzi huo wa mahakama haukuungwa mkono na jopo lote la majaji watatu.