Reports by trial

11.12.09 - ICTR/NTAWUKULILYAYO - NAIBU MKUU WA MKOA APANDA KIZIMBANI KUJITETEA MWENYEWE

Arusha, Desemba 11, 2009 (FH) - Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Mkoa nchini Rwanda, Dominique Ntawukulilyayo ambaye Jumanne wiki hii alipanda kizimbani kujitetea mwenyewe dhidi ya tuhuma za mauaji ya kimbari zinazomkabili, aliiambia Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwamba alikuwa anashirikiana vema na raia wenzake toka kabila la Watutsi bila kuwabagua.

11.12.09 - ICTR/NZABONIMANA - MAHAKAMA YAHAMIA RWANDA KUMSIKILIZA SHAHIDI MGONJWA NA MZEE

Arusha, Desemba 11, 2009 (FH) -Mahakama namba III ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) inayosikilza kesi dhidi ya aliyekuwa Waziri wa Vijana wa Rwanda, Callixte Nzabonimana Jumanne wiki hii ilihamia nchini Rwanda kwenda kupata ushahidi wa shahidi ambaye ni mzee na mgonjwa.

04.12.09 - ICTR/NZABONIMANA - MASHAHIDI 14 WATOA USHAHDI DHIDI YA WAZIRI WA ZAMANI WA VIJANA

Arusha, 04 Desemba, 2009 (FH) - Kesi pekee iliyokuwa ikiunguruma wiki hii mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ni kesi inayomhusu Waziri wa zamani wa Vijana nchini Rwanda, Callixte Nzabonimana.

27.11.09 - ICTR/NTAWUKULILYAYO - NAIBU MKUU WA MKOA KUJITETEA MWENYEWE DESEMBA 8

Arusha, 27 Novemba, 2009 (FH) - Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Mkoa nchini Rwanda, Dominique Ntawukulilyayo atapanda kizimbani kujitetea mwenyewe dhidi ya tuhuma za mauaji ya kimbari zinazomkabili, Desemba 8, 2009.

20.11.09 - ICTR/GATETE - AHITIMISHA KULETA MASHAHIDI WA KESI DHIDI YA MKURUGENZI WA ZAMANI WA RWANDA

Arusha, 20 Novemba, 2009 (FH) - Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu wiki hii alihitimisha kuleta jumla ya mashahidi wake 22 mahakamani katika kesi dhidi ya Mkurugenzi wa zamani wa Wizara ya Familia na Masuala ya Wanawake nchini Rwanda, Jean Baptiste Gatete. 

13.11.09 - ICTR/NZABONIMANA - ADAI MTUHUMIWA ALIKUWA ‘'MCHINJAJI WATU'' MKOANI GITARAMA

Arusha, 13 Novemba, 2009 (FH) - Kesi ya Waziri wa zamani wa Vijana nchini Rwanda, Callixte Nzabonimana iliyokwama kwa muda wa miezi 21 sasa, ilianza kusikilizwa Jumatatu wiki hii mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).

13.11.09 - ICTR/GATETE - SHAHIDI ADAI HUTUBA YA MKURUGENZI ILICHOCHEA MAUAJI DHIDI YA WATUTSI

Arusha, 13 Novemba, 2009 (FH) - Shahidi mmoja wa mashtaka katika kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya aliyekuwa Mkurugenzi katika wizara ya Familia na Masuala ya Wanawake nchini Rwanda, Jean Baptiste Gatete, Jumatano wiki hii alidai mahakamani kwamba hotuba ya uchochezi aliyoitoa mtuhumiwa huyo siku moja baada ya kifo cha Rais Juvenal Habyarimana, ilisababisha kufanyika kwa mauaji dhidi ya Watutsi katika mkoa wa Kibungo,  mashariki ya Rwanda.

02.07.09 - ICTR/NSHOGOZA - MWANASHERIA WA RWANDA ATIWA HATIANI LAKINI KAACHIWA HURU

Arusha, Julai 02, 2009 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Alhamisi imemhukumu kifungo cha miaka 10 jela mwanasheria wa Rwanda, Leonidas Nshogoza baada ya kumtia hatiani kwa kosa moja la kuidhalilisha mahakama.

01.05.09 - ICTR/NSHOGOZA - KESI YA KURUBUNI MASHAHIDI KWA HONGO YAHITIMISHWA

Arusha, Machi 01, 2009 (FH) - Pande zote mbili za utetezi na mashtaka katika kesi ya kurubuni mashahidi kutoa ushahidi wa uongo inayomkabili mwansheria wa Rwanda, Leonidas Nshogoza, zimehitimisha hoja zao za mwisho Jumatano wiki hii mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).

30.03.09 - ICTR/NSHOGOZA - WAKILI WA RWANDA AKANA KUFAHAMU KUWEPO KWA POSHO YA MASHAHIDI WA UTETEZI

Arusha, Machi 30, 2009 (FH) - Mwanasheria wa Rwanda anayekabiliwa na shitaka la kurubuni mashahidi wa utetezi kwa kuwapatia hongo, Leonidas Nshogoza amedai Jumatatu mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwamba hajawahi kuelezwa kamwe kuwapo kwa posho kwa ajili ya mashahidi wa utetezi katika mahakama hiyo.