Justice Info

Other reports

25.06.12 - ICTR/NDIMBATI - KESI YA SABA TOKA ICTR YAKUBALIWA KUHAMISHIWA RWANDA

Arusha, Juni 25, 2012,2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu ilikubali maombi ya mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo kuhamishia nchini Rwanda kesi ya mshitakiwa, Aloys Ndimbati.

26.06.12 - ICTR/BIZIMANA - ICTR YAHITIMISHA KUPOKEA USHAHIDI MAALUM KATIKA KESI YA BIZIMANA

Arusha, Juni 26, 2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu ilihitimisha upokeaji wa ushahidi maalum katika kesi inayomkabili mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ambaye bado anasakwa na mahakama hiyo, Augustin Bizimana, Waziri wa zamani wa Ulinzi waRwanda. ‘’Naomba niwajulishe kwamba upokeaji wa ushahidi maalum katika kesi ya Bizimana uliendelea leo (Jumatatu) asubuhi kwa kupata ushahidi kutoka kwa shahidi wa mwisho ambaye pia amehitimisha ushahidi wake leo.Hivyo basi kufuatia hatua hiyo, upokeaji ushahidi huo umehitimishwa,’’ alieleza Msemaji wa ICTR, Roland Amossouga. Bizimana anashitakiwa kwa makosa ya mauaji ya kimbari, kula njama kutenda makosa hayo, uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita. Kesi nyingine mbili za aina hiyo ambazo ushahidi wake umeshapokelewa ni pamoja na ile ya mtuhumiwa anayesakwa vikali na anayesadikiwa kuwa ndiyo mfadhili wa mauaji ya kimbari, Felicien Kabuga na Protais Mpiranya, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Walinzi wa   Rais. Utaratibu wa kupokea ushahidi katika kesi ya mshitakiwa ambaye bado hajakamatwa umewekwa ili kuhifadhi ushahidi husika uweze kutumika pindi mshitakiwa akitiwa mbaroni hapo baadaye. Wakili wa Zamu wa Bizimana, Yitiha Simbeye aliita jumla ya mashahidi watatu kwa ajili ya utetezi wa mteja wake. Utetezi katika kesi ya Biziamana ulianza Mei 14, 2012. NI © Hirondelle News Agency

15.06.12 - ICC/PROSECUTOR - BENSOUDA WA GAMBIA AAPISHWA MWENDESHA MASHITAKA MAPYA WA ICC

Arusha, Juni 15, 2012 (FH) – Rais wa Gambia, Fatou Bensouda Ijumaa aliapishwa kuwa Mwendesha Mashitaka mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) iliyopo The Hugue, Uholanzi, kuchukua nafasi ya Luis Moreno Ocampo kutokaArgentina, ambaye mkataba wake wa kazi wa miaka tisa umemalizika.

01.06.12 - SCSL/TAYLOR - RAIS WA ZAMANI WA LIBERIA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 50 JELA

Arusha, Juni 01,2012 (FH) – Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCS) Jumatano wiki hii imemhukumu kifungo cha miaka 50 jela Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor baada ya kumtia hatiani kwa mashitaka 11 yaliyokuwa yanamkabili ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

5.05.2012 – MAJUMUISHO YA WIKI (AUDIO)

Arusha, Mei 5, 2012 (FH) – Adhabu gani hii ya kifungo kwa Charles Taylor? Nani atashughulikia kesi ya Saif al-Islam Gaddafi? Yafuatayo ni matukio ya wiki juu ya haki ya kimataifa kama yanavyowasilishwa na Nicodemus Ikonko...

26.04.12 - SCSL/TAYLOR - MAHAKAMA YAMTIA HATIANI TAYLOR KWA KUSAIDIA UHALIFU SIERRA LEONE

Arusha, Aprili 26,2012 (FH) – Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCS) Alhamisi imemtia hatiani Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor kwa mashitaka yote 11 yaliyomkabili ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Imemtia hatiani hususan  kwa sababu ya kuwasaidia na kuwaunga mkono waaasi na siyo kwa kuamuru kutenda uhalifu huo.

25.04.12 - ICC/LUBANGA - ICC KUSIKILIZAJI MAPENDEKEZO YA ADHABU DHIDI YA LUBANGA JUNI 13

Arusha, Aprili 25, 2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) itasikiliza hoja za mapendekezo ya adhabu atakayopewa kiongozi wa zamani wa wanamgambo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga Juni 13, 2012.

24.04.12 - ICC/KENYA - KIBAKI ANG’ANG’ANA KUWASHITAKI KENYATTA NA WENZAKE NCHINI KENYA

Nairobi, Aprili 24,2012 (FH) – Rais Mwai Kibaki waKenya, amesema Jumanne alipokuwa analihutubia taifa ndani ya Bunge kwamba serikali yake bado inataka watuhumiwa wanne wa nchi hiyo wanaotakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu washitakiwe nchini humo.

24.04.12 - SCSL/TAYLOR - KESI YA TAYLOR KUTOLEWA HUKUMU APRILI 26

Freetown, Aprili 24,2012 (FH) – Ikiwa umepita zaidi ya mwaka mmoja tangu kesi dhidi ya kiongozi wa zamani waLiberia, Charles Taylor kuhitimisha hoja za mwisho mbele ya Mahakama Maalum yaSierra Leone (SCSL), sasa mahakama hiyo itatoa hukumu Alhamisi, Aprili 26.

25.04.12 - ICC/KATANGA - HOJA ZA MWISHO KESI YA KATANGA, NGUDJOLO KUANZA KUPOKEWA MEI 15

Arusha, Aprili 25, 2012 (FH) –Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) itasikiliza hoja za mwisho katika kesi inayowahusu viongozi wa waasi wawili wa Congo, GermainKatanga and Mathieu Ngudjolo, kati ya Mei 15 and 23, 2012.