16.03.12 - ICC/LIBYA - MAHAKAMA MAURITANIA KUAMUA JUU YA KUMHAMISHA AL-SENOUSSI

The Hague, Uholanzi, Machi 16, 2012 (FH) – Itakuwa ni jukumu la Mahakama nchiniMauritania kuamua kumhamishia nchi nyingine Kanali Abdullah Al-Senoussi, aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Taifa waLibya. Alitiwa mbaroni kwenye uwanja wa ndege wa Nouakchott Ijumaa iliyopita alipokuwa anawasili uwanjani hapo usiku akitokeaCasablanca akiwa na hati bandia ya kusafiria ya nchi yaMali.

 

 

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati ya kumkamati kiongozi huyo, Juni 27, 2011 kwa uhalifu dhidi ya binadamu. Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa ya ICC, al-Senoussi alikuwa ni mkuu wa Idara ya Usalama yenye nguvu kubwa na utendaji kazi kwa ufanisi katika utawala wa mabavu wa Gaddafi’’

Alitumia ‘’mamlaka yake ya kuyaongoza majeshi na kuyaamuru  kufanya mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya raia waliokuwa wanaandamana katika jiji laBenghazi.’’ 

 

Ufaransa naLibya, wote wameonyesha nia ya kutaka kushugulikia mashitaka dhidi ya yake.

Senoussi pia ameshawahi kupewa hati ya kimataifa ya kukamatwa iliyotolewa na Ufaransa mwaka 1999 mjiniParisna kumtia hatiani bila mwenyewe kuwepo mahakamani.Alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kujihusisha katika ulipuaji wa ndege ya UTA katika anga zaNiger, 1989, ambapo watu 170 walikufa wakiwemo raia 54 wa Ufaransa.

 

‘’Mahakama zetu ni nzuri sana na hata ni bora zaidi hususan ni mjini Tripoli na tunaweza kuendesha kesi yake kwa mujibu wa viwango vya kimataifa,’’ Waziri wa Sheria wa Libya, Ali Hmeida Ashur alisema Jumapili.

NchiniLibyaal-Senoussi pia anashitakiwa kwa ‘’mashitaka ya uhalifu ikiwa ni pomoja na matumizi mabaya ya fedha za umma na mamlaka.’’ Ujumbe waLibyaunatarajiwa kuwasiliNouakchottwiki hii.

Mauritaniahaijaridhia Mkataba wa Roma na hivyo haiwajibiki kushirikiana na ICC.

 

NI/SM/GF

© Hirondelle News Agency