25.04.12 - ICC/KATANGA - HOJA ZA MWISHO KESI YA KATANGA, NGUDJOLO KUANZA KUPOKEWA MEI 15

Arusha, Aprili 25, 2012 (FH) –Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) itasikiliza hoja za mwisho katika kesi inayowahusu viongozi wa waasi wawili wa Congo, GermainKatanga and Mathieu Ngudjolo, kati ya Mei 15 and 23, 2012. 

 

Kwa mujibu wa taarifa ya ICC iliyotolewa Jumanne, upande wa mashitaka ndio utakaoanza kuwasilisha majumuisho, ukifuatiwa na wawakilishi wa waathirika, ambapo utetezi utamalizia. Majaji pia, taarifa hiyo inasema, watakuwa na nafasi ya kuuliza maswali kwa pande zote. 

Uwasilishwaji wa hoja hizo unakuja baada ya majaji wanaosikiliza kesi hiyo kutembelea eneo la Ituri lililoko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo(DRC), kati ya Januari 16 na 20, 2012, ili kuchekecha ushahidi uliotolewa. 

Majaji hao walisafiri hadi vitongoji vya Bogoro, Aveba, Zumbe na Kambusto, kujionea maeneo ambayo yanadaiwa uhalifu ulitendeka na vijiji wanakotoka washitakiwa na mashahidi. 

Jopohilola majaji liliamua kuwa ilikuwa ni muhimu kutembelea maeneo hayo, pamoja na waendesha mashitaka, mawakili wa utetezi na wawakilishi wa waathirika wa uhalifu huo ili kuwawezesha kufikia maamuzi sahihi juu ya ushahidi uliotolewa. 

Katangana Ngudjolo wanashitakiwa kwa makosa ya uharifu dhidi ya binadamu na yale ya kivita, hususani kufuatia uhusika wao katika mashambulizi eneo la Bogoro mnamo Februari 24, 2003 ambapo watu zaidi ya 200 wliuwawa.

Kesiyaoilianza kusikilizwa Novemba 24, 2009.Katangaalikamatwa na kuhamishiwa The Hague Octoba 17, 2007, na Ngudjolo alitiwa mbaroni Februari 6, 2008 na kupelekwa katika mahabusu ya mahakama hiyo siku moja baadaye.

FK/NI

© Hirondelle News Agency