24.04.12 - ICC/KENYA - KIBAKI ANG’ANG’ANA KUWASHITAKI KENYATTA NA WENZAKE NCHINI KENYA
Nairobi, Aprili 24,2012 (FH) – Rais Mwai Kibaki waKenya, amesema Jumanne alipokuwa analihutubia taifa ndani ya Bunge kwamba serikali yake bado inataka watuhumiwa wanne wa nchi hiyo wanaotakiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu washitakiwe nchini humo.
Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, Mbunge William Ruto, Katibu Mkuu wa zamani wa Baraza la Mawaziri, Francis Muthaura na mwandishi wa habari, Joshua Arap Sang, wanashitakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kuhusika kwao na ghasia zilizofanyika baada ya uchaguzi 2007/2008 na kusababisha watu wapatao 1,000 kuuawa na maelfu kukosa mahali pa kusihi.
‘’Ninafahamu ni kiasi gani kesi hizi za ICC zinawagusa Wakenya. Pia ninafahmu kwamba Bunge hili limepitisha azimio la kuitakaKenyakujitoa kwenye ICC.Waathirika wa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wanastahili kutendewa haki.Lakini pia Wakenya wanaokabiliana na mashitaka hayo wanastahili usikilizaji wa haki wa kesiyao,’’ alitamka.
Alisema kwamba serikali ‘’inaangalia uwezekano wa kuwa na chombo cha ndani kushughulikia uhalifu wowote wa kimataifa.’’ Hata hivyo bado hakujatangazwa uwepo wa chombo chochote cha aina hiyo.
ICC imechukua kesi za Wakenya hao baada ya nchi hiyo kushidnwa kuanzisha mahakama maalum kushughulikia kesi hizo.
Kenyakwa ujumla wake na Bunge wamepata mkanganyo mkubwa juu ya mipango ya watuhumiwa wawili wa ICC-Kenyatta na Ruto kutaka kuwania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu hapo mwakani.Baadhi ya mawaziri wanataka wawili hao wagombee nafasi hiyo huku wengine wakiwataka kuachana na adhma hiyo.
NI/BB/GF
© Hirondelle News Agency
