25.04.12 - ICC/LUBANGA - ICC KUSIKILIZAJI MAPENDEKEZO YA ADHABU DHIDI YA LUBANGA JUNI 13

Arusha, Aprili 25, 2012 (FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) itasikiliza hoja za mapendekezo ya adhabu atakayopewa kiongozi wa zamani wa wanamgambo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga Juni 13, 2012.

 

Machi 14, mwaka huu, ICC iliyopo The Hague, Uholanzi, ilimtia hatiani Lubanga (51) kwa mashitaka ya kuwasajili na kuwatumia watotokamaaskari katika mapambano ya silaha katika eneo lenye utajiri wa dhahabu wakati wa vita vya kumwaga damu vilivyodumu kwa miaka minne katika wilaya ya Ituri, eneo la Mashariki mwa DRC kati ya Septemba 1, 2002 na Agosti 13, 2003.

Mwendesha Mashitaka na mawakili wa walioathirika na uhalifu huo wanatakiwa kuwasilisha vielelezo muhimu vilivyotolewa wakati wa usikilizaji wa kesi, ambavyo vinaweza kusadia katika kufikia aina ya  adhabu, ifikapo Mei 14, 2012.

Pande hizo mbili pia zinatakiwa kuwasilisha maoniyaojuu ya adhabu muafaka anayostahili kupewa Lubanga, wakizingatia pamoja na mambo mengine, mazingira halisi ya kesi yenyewe.

Upande wa utetezi nao unatakiwa kujibu hoja husika ifikapo Mei 28, 2012 na pia unaweza kuomba kibali cha kuwasilisha ushahidi mpya wakati wa usikilizaji wa mapendekezo ya adhabu.

Jopo la majaji watatu waliosikiliza kesi hiyo walikubaliana kwa kauli moja kwamba Lubanga alishiriki katika ‘’Mpango wa kuanzisha jeshi’’ ili kuthibiti Ituri kisiasa na kijeshi.

Mpango huo, walihitimsiha, ndiyo uliwasajili watoto wa chini ya miaka 15 katika kundi la waasi la UPC na tawi lake la kijeshi lijulikanalokamaFPLC. Lubanga ndiye aliyekuwa Rais wa UPC wakati huo.

Lubanga alitiwa mbaroniKinshasamwaka 2005 na kisha kuhamishiwa ICC, The Hague March 2006. Kesi yake ilianza kusikilizwa Januari 26, 2009.

NI/FK/GF


© Hirondelle News Agency