26.04.12 - SCSL/TAYLOR - MAHAKAMA YAMTIA HATIANI TAYLOR KWA KUSAIDIA UHALIFU SIERRA LEONE
Arusha, Aprili 26,2012 (FH) – Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCS) Alhamisi imemtia hatiani Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor kwa mashitaka yote 11 yaliyomkabili ikiwa ni pamoja na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Imemtia hatiani hususan kwa sababu ya kuwasaidia na kuwaunga mkono waaasi na siyo kwa kuamuru kutenda uhalifu huo.
Mahakama iliyokuwa inaongozwa na Jaji Richard Lussick imebaini kwambaTayloralilipatia kundi la waasi la RUF nchiniSierra Leonemisaada ya kijeshi, kioperesheni na fedha huku akijua kwamba walikuwa wanatenda uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na mauaji, ubakaji,utumwa wa ngono,kuwasajili na kuwatumia watoto chini ya miaka 15 katika mapambano.
Hukumu hiyo ilikuwa inatolewa toka mjini The hague, Uholanzi na kurushwa moja kwa moja kwa mtandao wa intaneti.
Mahakama imepanga Mei 16 kusikilizaji mapendekezo ya adhabu ambapo Mei 30 ndipo adhabu yenyewe itakapotamkwa na mahakama hiyo.
Kesi yake ilianza kusikilizwa Juni 2007. Mwendesha mashitaka iliita mashahidi 94 wakiwemo 32 ambao walikuwa ni marafiki wa karibu waTaylorambao hatimaye walitoa ushahidi dhidi yake.
Tayloraliandaliwa mashitaka Juni 2003 lakini hati ya kukamatwa kwake ilibakia kuwa siri hadi alipokubali kuachia madaraka Agosti 2003, bada ya kupewa hifadhi ya ukimbizi wa kisiasa nchiniNigeria. Machi 2006, alitiwa mbaroni nchiniNigeriana kisha kusafirishwa hadi katika mahakama ya SCSL.
Serikali ya Uholanzi ilikubali kupokea kesi hiyo kusikiliziwa nchini mwake kufuatia ombi la Rais waLiberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye alikuwa anahofia kuzuka kwa ghasia iwapo kesi hiyo ingesikilizwaSierra Leone.
NI/ER/JC
© Hirondelle News Agency
