Other reports
01.03.12 - SCSL/TAYLOR - KESI TAYLOR KUTOLEWA HUKUMU APRILI 26
The Hague,Machi 1, 2012 (FH) - Mahakama Maalum ya Sierra Leone (SCSL) iliyopo The Hague, Uholanzi,itatoa hukumu ya kesi inayomkabili Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor Aprili 26, mwaka huu.
24.02.12 - MAJUMUISHO YA WIKI - WIGO WA UCHUNGUZI UHALIFU IVORY COAST WAONGEZWA
Arusha, Februari 24, 2012 (FH) - Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imeamua kuongeza wigo wake wa kufanya uchunguzi wa uhalifu nchini Ivory Coast kwa kuongeza tuhuma zilizodaiwa kufanyika kati ya Septemba 19, 2002 na Novemba 28, 2010, Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imeamua kuhamishiwa nchini Rwanda kesi ya mtuhumiwa ambaye bado anasakwa na mahakama hiyo, Fulgence Kayishema.
24.02.12 - WIKI IJAYO - KESI DHIDI YA BEMBA KUENDELEA KUUNGURUMA WIKI IJAYO ICC
Arusha, Februari 24, 2012 (FH) - Usikilizaji wa kesi ya kiongozi wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congpo (DRC), Jean Pierre Bemba unaendelea wiki ijayo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC) wakti katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) hakutakuwapo na usikilizaji wa kesi baada kesi pekee iliyokuwa inasikilizwa ya Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda, Augustin Ngirabatware kuahirishwa hadi Machi 5.
17.02.12 - MAJUMUISHO YA WIKI - RAIS MPYA ICTR,RWANDA YAUNDA MAHAKAMA YA WAHALIFU WA KIMATAIFA
Arusha, Februari 17, 2012 (FH) - Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wiki hii wamewachagua viongozi wa ngazi ya juu wa mahakama hiyo wakiwemo Rais na Makammu wake huku Rwanda ikiwa imeunda Mahakama Maalum kwa ajili ya kushughulikia wahalifu wa kimataifa.
17.02.12 - WIKI IJAYO - KESI DHIDI YA NGIRABATWARE NA BEMBA KUUNGURUMA WIKI IJAYO
Arusha, Februari 17, 2012 (FH) - Kesi za Augustin Ngirabatware na Jean-Pierre Bemba zitaendelea kusikilizwa katika mahakama mbili tofauti wiki ijayo.
03.02.12 - MAJUMUISHO - KESI ZA BEMBA NA NGIRABATWARE ZAANZA TENA KUSIKILIZWA
Arusha, Februari 03, 2012 (FH) - Usikilizaji wa kesi umeanza tena mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ambapo kesi ya Jean Pierre Bemba ilianza tena kuunguruma huku kesi ya Waziri wa zamani wa Mipango wa Rwanda, Augustin Ngirabatware ikiendelea pia mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).
03.02.12 - WIKI IJAYO - KESI YA BEMBA KUENDELEA KUSIKILIZWA ICC WIKI IJAYAO
Arusha, Februari 03, 2012 (FH) - Usikilizaji wa kesi ya Jean Pierre Bemba unaendelea wiki ijayo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wakati katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) hakutakuwapo usikilizaji wa kesi.
27.01.12 - MAJUMUISHO - WAKENYA WANNE WANA KESI YA KUJIBU ICC,MUGESERA ATUA RWANDA
Arusha, Januari 27, 2012 (FH) - Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imewakuta Wakenya wanne kati ya sita kuwa wana kesi ya kujibu kutokana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo kati ya 2007 na 2008, mwanasiasa wa Rwanda, Leon Mugesera arejeshwa nchini mwake kutoka Canada.
27.01.12 - WIKI IJAYO - ICTR YAANZA KUSIKILIZA KESI,MUGESERA HUENDA AKAFIKISHWA MAHAKAMANI RWANDA
Arusha, Januari 27, 2012 (FH) - Baada ya mapumziko ya muda mrefu kesi moja itaanza kusikilizwa tena Jumatatu ijayo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wakati Leon Mugesera aliyerejeshwa nchini Rwanda wiki hii anaweza kufikishwa mbele ya jaji nchini humo.
20.01.12 - MAJUMUISHO - WALUMBANA UHAMISHO WA UWINKINDI, BAN ATEUA MSAJILI
Arusha, Januari 20, 2012 (FH) - Wakati kumezuka malumbano makali kati ya viongozi waandamizi wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) juu ya kucheleweshwa kupelekwa Rwanda mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari, mchungaji Jean Uwinkindi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) amemteua raia wa Australia kuwa Msajili wa chombo kitakachorithi kazi za Mahakama mbili za Umoja huo.
