Other reports

20.01.12 - WIKI IJAYO - UAMUZI WA WATUHUMIWA WA KENYA WIKI IJAYO, KESI YA BEMBA JUMATATU

Arusha, Januari 20, 2012 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) inatarajiwa wiki ijayo kutangaza uamuzi wa uthibitisho wa tuhuma ya kesi ya Wakenya sita maarufu wanaodaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu baada ya uchuguzi kati 2007 na 2008 na kesi ya muasi mmoja wa Jamhuri ya Kidemoktrasia ya Congo (DRC) Jean Pierre Bemba inaendelea kusikilizwa Jumatatu ijayo.

13.01.12 - WIKI IJAYO - KESI KUANZA KUSIKILIZWA TENA ICC WIKI IJAYO

Arusha, Januari 13, 2012 (FH) - Mwezi mmoja baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) itaanza shughuli zake rasmi wiki ijayo, huku Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) nayo itaendelea na kazi zake ifikapo mwishoni mwa Januari, mwaka huu.

13.01.12 - MAJUMUISHO - RPF WASAFISHWA KUTUNGUA NDEGE YA RAIS, MUGESERA ASITISHWA KUREJESHWA RWANDA

Arusha, Januari 13, 2012 (FH) - Wakati ripoti ya timu ya wataalamu wa Ufaransa Jumanne wiki hii imelisafisha Kundi la Waasi wa zamani nchini Rwanda (RPF) kwamba halikuhusika na tukio la kutungua ndege iliyomchukua Rais Juvernal Habyarimana wa nchi hiyo Aprili 6, 1994 na kusababiusha kifo chake, mpango wa kumrejesha nchini Rwanda mtuhumiwa wa siku nyingi wa mauaji ya kimbari Leon Mugesera umesitishwa kwa muda.

23.12.11 - MAJUMUISHO - VIGOGO WA MRND JELA MAISHA,MBARUSHIMANA AACHIWA HURU

Arusha, Desemba 23, 2011 (FH) - Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imewahukumu vifungo vya maisha jela wanasiasa wawili wakongwe wa Rwanda, majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC) wametupilia mbali ombi la mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo kupinga kuachiwa huru kwa mtuhumiwa Callixte Mbarushimana.

16.12.11 - WIKI IJAYO - HUKUMU YA VIONGOZI WAKUU WA MRND JUMATANO IJAYO

Arusha, Desemba 16, 2011 (FH) - Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda(ICTR) Jumatano ijayo itatoa hukumu ya kesi inayosubiriwa kwa hamu ya viongozi wakuu wa zamani wa chama tawala nchini Rwanda cha MRND, wiki ijayo hakutakuwepo usikilizaji wa kesi katika Mahakama ya Kiamtaifa ya Uhalifu (ICC) iliyopo The Hague,Uholanzi, kutokana na watumishi wake kwenda likizo ya mwisho wa mwaka.

16.12.11 - MAJUMUISHO YA WIKI - BAGOSORA, NSENGIYUMVA WAPUMUA , MGAMBIA AWA BOSI ICC

Arusha, Desemba 16, 2011(FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wiki hii imepunguza adhabu walizopewa Wanyarwanda watatu baada ya kutiwa hatiani kwa kuhusika kwao katika mauaji ya kimbari akiwemo Kanali Theoneste Bagosora, huku Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ikiwa imepata mwendesha mashitaka mpya, Fatou Bensouda toka nchini Gambia.

10.12.11 - MAJUMUISHO - GBAGBO MBELE YA ICC, AOMBA NIZEYIMANA AFUNGWE MAISHA

Arusha, Desemba 10, 2011 (FH) - Wakati Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo amefikishwa kwa mara ya kwanza mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) wiki hii, mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ameiomba Mahakama hiyo impatie adhabu ya kifungo cha maisha jela, afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda, Kapteni Idelphonse Nizeyimana.

10.12.11 - WIKI IJAYO - HUKUMU YA RUFAA YA BAGOSORA WIKI IJAYO, ICC KUPATA MWENDESHA MASHITAKA MPYA

Arusha, Desemba 10, 2011 (FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) wiki ijayo inatarajiwa kutoa hukumu za kesi mbili za rufaa, ikiwemo ya mtu anayesadikiwa ndiye mpangaji mkuu wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Kanali Theoneste Bagosara na kusikiliza kesi nyingine mbili za rufaa. Katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) nchi wananchama watachagua majaji na mwendesha mashitaka mpya wa mahakama hiyo.

02.12.11 - MAJUMUISHO - GBAGBO ATINGA ICC, BENSOUDA KUMRITHI OCAMPO

Arusha, Desemba 2, 2011 (FH) - Wakati Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo alihamishiwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliyopo The hague, Uholanzi,Juamatano wiki hii, Fatou Bensouda, raia wa Gambia atachukua nafasi mpya ya Mwendesha Mshitaka wa ICC, itakayoachwa wazi baada ya Luis Moreno Ocampo wa sasa kumaliza muda wake.

21.11.11 - ICTR/BIZIMANA - ICTR YAANZA KUPOKEA USHAHIDI MAALUM KESI YA BIZIMANA

Arusha, Novemba 21, 2011 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu wiki hii imeanza kupokea kwa faragha ushahidi maalum  utakaohifadhiwa na kutumika baadaye pindi akikamatwa  aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Rwanda, Augustin Bizimana ambaye bado anasakwa vikali na mahakama hiyo.