Justice Info

ICC

15.03.12 - ICC/LUBANGA - DUNIA YASIFIA HUKUMU DHIDI YA LUBANGA

Arusha, Machi 15, 2012 (FH) - Marekani imeungana na mashirika ya kimataifa na nchi mbalimbali duniani kuipongeza hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC) kumtia hatiani kwa uhalifu wa kivita Kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga na kuiita hukumu hiyo kuwa ‘'ni ya kihistoiria.''

14.03.12 - ICC/LUBANGA - ICC YAMTIA HATIANI LUBANGA KWA KUWATUMIA WATOTO KWENYE MIPIGANO

The Hague, Uholanzi, Machi 14, 2012 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Jumatano imetia hatiani Kiongozi wa zamani wa Wanamgambo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC),Thomas Lubanga kwa kuwasajili na kuwatumia watoto wa chini ya miaka 15 kwenye mapigano,eneo la Ituri, Mashariki mwa DRC, kati ya Septemba 2002 na Agosti 2003.

29.02.12 - ICC/LUBANGA - ICC KUTOA HUKUMU YA KESI YAKE YA KWANZA MACHI 14

The Hague,Februari 29, 2012 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliyopo The Hague, Uholanzi, itatoa hukumu yake ya kwanza katika kesi inayomkabili, Kiongozi wa zamani wa waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga Machi 14, mwaka huu.

24.01.12 - ICC/KENYA - ICC YATHIBITISHA TUHUMA DHIDI YA WAKENYA WANNE

Arusha, Januari 24, 2012 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Jumatatu ilithibitisha kwamba watuhumiwa wanne wa Kenya kati ya sita, wana kesi ya kujibu mbele ya mahakama hiyo juu ya mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.

15.09.11 - ICTR/MWENDESHA MASHITAKA - JALLOW ATEULIWA TENA KUENDELEA NA WADHIFA WAKE ICTR

Arusha, Septemba 15, 2011 (FH) - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatano limemteua tena Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Hassan Bubacar Jallow kuendelea na wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

18.04.08 - ICC/ARBIA MAHOJIANO - MSAJILI MPYA WA ICC ASHUTUMU KUHITIMISHA KAZI ZA ICTR HARAKA

Arusha, Aprili 18, 2008 (FH) – Msajili mpya wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), Sylvana Arbia alifanya mahaojiano maalum na Shirika la Habari la Hirondelle kuhusu mtazamo wake juu ya mahakama hiyo ya dunia pamoja na kazi yake ya awali ya Mkuu wa Waaendesha Mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), kabla ya kuchukua rasmi nafasi yake mpya hivi karibuni. Yafuatayo ni mahojiano yenyewe… Swali: Kitu gani cha kwanza kinachokujia kichwani mwako ambacho unataka kufanya ICC? Jibu: Kwanza ningependa kutathmini idadi ya wafanyakazi waliopo kwa lengo la kujaza nafasi zilizoachwa wazi ili kuongeza ufanisi wa kazi ambao ni muhumu sana katika menejementi ya mahakama na kuimarisha kitengo cha Huduma za Mahakama kwa kutumia utaalamu wa kisasa kwa kuangalia kwa makini kesi ya kwanza ambayo inatarajiwa kuanza kusikilizwa mwaka huu.