Justice Info

ICTR

30.11.12 - MAJUMUISHO YA WIKI - POLISI WA UJERUMANI WAMKOSA KABUGA 2007,MWENDESHA MASHITAKA NORWAY ATAKA MTUHUMIWA AFUNGWE MIAKA 21 JELA

Arusha, Novemba 30, 2012 (FH) – Jarida moja la kila wiki la Ufaransa limechapisha habari kwamba polisi nchini Ujerumani walimkosa kumtia mbaroni mwaka 2007, mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda anayesakwa vikali, Felician Kabuga huku Mwendesha mashitaka nchini Norway ameiomba mahakama impatie kifungo cha miaka 21 jela mfanyabiashra mmoja wa Rwanda kwa kushiriki kwake katika mauaji ya kimbari mwaka 1994.

05.10.12 - ICC/LUBANGA - MWENDESHA MASHITAKA, MAWAKILI WA UTETEZI WAKATA RUFAA KESI YA LUBANGA

Arusha, Oktoba 05, 2012 (FH) – Pande zote mbili, za utetezi na mwandesha mashitaka katika kesi ya kiongozi wa zamani wa wanamgambo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Thomas Lubanga, zimekata rufaa kupinga adhabu aliyopewa mshitakiwa huyo ya kifungo cha miaka 14 jela.

25.09.12 - ICTR/ACHPR - KAMISHENI YA AFRIKA KUSIMAMIA USIKILIZAJI WA KESI ZA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA

Arusha, September 25, 2012(FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imehitimisha majadiliano na Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) ili kusimamia usikilizaji wa kesi za mauaji ya kimbari zinazopelekwa kusikilizwa nchini Rwanda.

20.09.12 - ICTR/CASES - ATAKA WAFUNGWA WAWILI WAONGEZEWE MAKOSA

Arusha, Septemba 20,2012 (FH) – Mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ameiomba mahakama hiyo iwatie hatiani kwa tuhuma nyingine walizoachiwa huru wafungwa wawili, akiwemo Waziri wa zamani wa Vijana wa Rwanda, Callixte Nzabonimana na afisa wa zamani wa jeshi la nchi hiyo, Ildephonse Nizeyimana.

12.09.12 - ICTR/GOVERNMENT II - MAHAKAMA YA RUFAA KUSIKILIZA KESI YA MAWAZIRI WAWILI OKTOBA 8

Arusha, Septemba 12, 2012 (FH) – Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) itasikiliza kesi ya rufaa  inayowakabili mawaziri wawili wa zamani wa Rwanda, Justin Mugenzi na Prosper Mugiraneza Oktoba 8, 2012.

06.09.12 - UN/MICT - BARAZA LA USALAMA LA UN KUAMUA HATMA YA KUMBUKUMBU ZA ICTR

Arusha, Septemba 06,2012 (FH) – John Hocking, Msajili wa Taasisi ya Kimataifa itakayorithi kazi za Mahakama za Kimataifa (MICT), Jumanne aliliambia Shirika la Habari la Hirondelle kwamba hatma ya mahali pa kuhifadhi kumbukumbu za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iko mikononi mwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

24.08.12 – MAJUMUISHO YA WIKI (AUDIO)

Arusha, Agosti 24, 2012 (FH) – Kesi ya Seif Al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya sasa itasikilizwa nchini humo. Senegal na Umoja wa Afrika (AU) zimetiliana saini kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Chad, Hissene Habre.Habari zaidi na Nicodemus Ikonko.

17.08.12 – MAJUMUISHO YA WIKI (AUDIO)

Arusha, Agosti 17, 2012 (FH) – Vyama vya upinzani dhidi ya serikali ya Rwanda vilivyopo uhamishoni kwa kushirikiana na vyama vya kirai vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ijumaa wamewasilisha maombi mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuwashitaki marais watatu wa Nchi za Maziwa Makuu.Katika mahakama hiyo pia Jenerali mstaafu wa jeshi amepanda kizimbani kumtetea kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la DRC, Jean Pierre Bemba. Habari zaidi na Nicodemus Ikonko.

14.08.12 - ICC/BEMBA - JENERALI WA UFARANSA UTOA USHAHIDI WA KITAALAMU KATIKA KESI YA BEMBA

Arusha, Agosti 14, 2012 (FH) – Shahidi wa kwanza wa utetezi katika kesi inayomkabli Jean Pierre Bemba mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) alisimama kizimbani Jumanne kama mtaalamu wa Kijeshi.

08.08.12 - MICT/REFERALS - WAKILI WA TANZANIA ADAI MAJAJI WA RWANDA WANAWEZA KUPENDELEA

Arusha, Agosti 08, 2012 (FH) – Upande wa utetezi katika kesi inayomkali mtuhumiwa ambaye bado anasakwa, Pheneas Munyarugarama ameiomba Mahakama ya Rufaa ya taasisi inayorithi kazi za Mahakama za Umoja wa Mataifa, MICT, tawi la Arusha,kubadili uamuzi wa kuipeleka kesi ya mteja wao kusikilizwa nchini Rwanda kwa madai kuwa majaji wa nchi hiyo hawatamtendea haki mtuhumiwa huyo.

Dossiers