ICTR/UNO
09.07.09 - ICTR/UN - ICTR SASA KUHITIMISHA KAZI ZAKE 2010
Arusha, Julai 9, 2009 (FH) - Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeiongezea muda wa mwaka mmoja Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kuhitimisha kazi zake.
07.07.09 - ICTR/WAFANYAKAZI - WAFANYAKAZI 350 WA ICTR KUPUNGUZWA KAZI IFIKAPO SEPTEMBA
Arusha, Julai 07, 2009 (FH) - Wafanyakazi 350 wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ikiwa karibu asilimia 30 ya wafanyakazi wote watakuwa wamepunguzwa kazi ifikapo Septemba 30, mwaka huu huku baadhi yao tayari wameshapata barua zao za notisi ya kuachishwa tangu wiki iliyopita.
12.06.09 - ICTR/UN - MAHAKAMA YA RUFAA YA ICTR KUENDELEA HADI 2013
Arusha, Juni 12, 2009 (FH) - Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Jaji Dennis Byron amewaeleza wafanyakazi wa Mahakama hiyo Ijumaa kwamba Mahakama ya Rufaa ya Mahakama hiyo inatarajiwa kuendelea na kazi zake hadi ifikapo katikati ya mwaka 2013.
03.06.09 - ICTR/UN - MWENDESHA MASHTAKA WA ICTR ASHUTUMIWA KWA KUTOWASHTAKI MAAFISA WA RPF
Arusha, Juni 03, 2009 (FH) - Shirika moja la Kupigania Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) lenye makao yake makuu mjini New York, Jumatatu limemshutumu Mwendesha Mshtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwa kushindwa kuwafikisha mahakamani maafisa waandamizi wa zamani wa Kundi la Waasi la RPF ambao sasa ni watawala wa Rwanda kukabiliana na tuhuma za uhalifu wa kivita waliodaiwa kufanya nchini humo mwaka 1994.
27.03.09 - ICTR/UN - WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KIMBARI HAWATAKWEPA MKONO WA SHERIA
Arusha, Machi 27, 2009 (FH) - Mkuu wa Idara ya Sheria wa Umoja wa Mataifa, Patricia O'Brien amesema watuhumiwa wote wa mauaji ya kimbari ambao watakuwa bado hawajatiwa mbaroni wakati Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) itakapohitimisha kazi zake watashughulikiwa na chombo kinachotarajiwa kuundwa kabla ya kufungwa kwa mahakama hiyo.
23.02.09 - ICTR/UMOJA WA MATAIFA - BAN KI-MOON KUTEMBELEA ICTR KWA MARA YA KWANZA IJUMAA WIKI HII
Arusha, 23 Februari 2009 (FH) - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ambaye atakuwa katika ziara barani Afrika wiki hii, Ijumaa atatembelea pia Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo Oktoba 2006.
16.12.08 - ICTR/UN - MAJAJI SABA WA ICTR KUACHIA NGAZI MWISHONI MWA MWAKA HUU
Arusha, Desemba 16, 2008 (FH) - Majaji saba kati ya 18 wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) watakuwa wamejiuzulu ifikapo Desemba 31, mwaka huu na kuiacha mahakama hiyo katika ukakasi mkubwa wa utekelezaji wa kazi zake.
16.10.08 - ICTR/BARAZA KUU - ICTR KUTOA HUKUMU DHIDI YA KESI 38 KATIKA KIPINDI CHA MIEZI 14 IJAYO
Arusha, Oktoba 16, 2008 (FH) - Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) inatarajia kutoa hukumu dhidi ya kesi 38 katika kipindi cha miezi 14 ijayo kabla ya kuhitisha rasmi kazi zake mwishoni mwaka ujao, kwa mujibu wa Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Dennis Byron.
26.09.08 - ICTR/UN - UJUMBE WA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUTEMBELEA ICTR WIKI IJAYO
Arusha, Septemba 26, 2008 (FH) - Ujumbe wa watu 11 kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa utatembelea Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) mjini Arusha kwa siku mbili kuanzia Jumatatu ijayo kutathmini kazi za mahakama hiyo ambayo inakaribia kuhitimisha, Shirika la Habari la Hirondelle limeripoti.
06.06.08 - ICTR/UN - MWENDESHA MASHTAKA WA ICTR AKIRI KUHUSIKA KWA RPF KATIKA MAUAJI
Arusha, Juni 6, 2008 (FH) - Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Hassan Jallow kwa mara ya kwanza amethibitisha kwamba baadhi ya askari wa Kundi la zamani la Waasi la RPF walishiriki katika mauaji mwaka 1994 nchini humo.
