Finances

12.05.06 - ICTR/FINANCES - GHARAMA ZA ICTR KUFIKIA DOLA BILIONI MOJA IFIKAPO 2007

Arusha, Mei 10, 2006 (FH) - Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, (ICTR) ametoa waraka kwa shirika la Habari la Hirondelle hapa kwamba gharama za kuendesha mahakama hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1995 hadi itakapofika 2007 zitafikia dola za Marekani bilioni moja, sawa na zaidi ya shilingi bilioni 1,000 za Tanzania. Mahakama hiyo ina makao yake makuu katika jijini Arusha, Kaskazini mwa Tanzania na ina jumla ya wafanyakazi wapatao 1,000 waliogawanywa katika idara makubwa tatu ikiwa ni pamoja na mahakama yenyewe, ofisi ya mwendesha mashtaka na ofisi ya Msajili.

Dossiers