Karera

07.12.07 - ICTR/KARERA - GAVANA WA ZAMANI WA KIGALI AKATIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA

Arusha, 7 Decemba 2007 (FH) - François Karera, 58, gavana wa zamani wa Kigali wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, alikatiwa Ijumaa kifungo cha maisha na mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya Rwanda(ICTR). Ofisa alikutwa na hatia ya mashtaka ya mauaji ya kimbari, makosa ya jinai kwa mujibu wa mashtaka wakati wa kufungua kesi yake Januari9, 2006.

28.11.06 - ICTR/KARERA - MWENDESHA MASHTAKA AOMBA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KARERA

Arusha, 27 Novemba 2006 (FH) – Mwendesha mashtaka katika Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji za Rwanda (ICTR) ameiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya maisha kwa François Karera kwa kesi ya mauaji yaliyofanyika mwaka1994. Karera, mwenye umri wa miaka 67, alikuwa gavana wa Kigali vijijini .

28.11.06 - ICTR/KARERA - KARERA AKILI KUTOKUWA NA HATIA

Arusha, Novemba 24, 2006 (FH) –François Karera, Gavana wa zamani wa Kigali vijijini nchini Rwanda amekili kutokua na hatia katika kesi ya mauaji iliyokua inamkabili na kuiomba Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia Kesi za Mauaji ya Rwanda (ICTR) kutoa uamuzi. Karera alitoa ombi hilo wakati kesi yake ilipokua ikisikilizwa kwa mara ya mwisho na kusubiri uamuzi wa majaji utakaotolewa baada ya uamuzi huo kukamilika.

08.05.06 - ICTR/KARERA - MKUU WA ZAMANI WA MKOA WA KIGALI VIJIJINI AANZA KUJITETEA ICTR

Arusha, Mei 8, 2006 (FH) - Mkuu wa zamani wa mkoa wa Kigali Vijijini, nchini Rwanda, François Karera, alianza kujitetea mwishoni mwa wiki dhidi ya tuhuma za mauaji ya kimbari zinazomkabili mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR). Kesi ya Karera ilianza kusikilizwa Januari, 2006 baada ya kukakaa katika mahabusi ya mahakama hii mjini hapa kwa muda wa zaidi ya miaka minne.

07.02.06 - ICTR/KARERA - MWENDESHA MASHTAKA AHITIMISHA KESI DHIDI YA KARERA

Arusha, Februari 3, 2006 (FH) - Mwendesha mashtaka katika kesi inayomkabili mkuu wa zamani wa mkoa wa Kigali Vijijini, François Karera, amehitimisha kesi yake Alhamisi wiki hii katika Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) baada ya kuita mashahidi 18 kuunga mkono mashtaka yake dhidi za mtuhumiwa. Kesi hiyo imesikilizwa kwa muda mfupi tu wa siku 16 kuanzia Januari 9, mwaka huu.

20.01.06 - ICTR/KARERA - SHAHIDI ADAI KARERA ALIPOKEA NA KUGAWA SILAHA KUULIA WATUTSI

Arusha, Januari 18, 2006(FH)-Shahidi mmoja wa upande wa mashtaka ameimbia Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwamba mkuu wa zamani wa mkoa wa Kigali Vijijini, François Karera, alipokea silaha Aprili 1994 zilizotumika kwa mauaji ya watu wa kabila la Kitutsi katika tarafa kadhaa zilizoko mkoani humo. Shahidi huyo wa tano kutoka wilaya ya Nyarugenge alisema Karera alifuatana na yeye pamoja na viongozi wenzake kupokea bunduki na risasi katika wizara ya Ulinzi mjini Kigali, Aprili 16.

18.01.06 - ICTR/KARERA - SHAHIDI AHUSISHA WALINZI WA KARERA NA MAUAJI

Arusha, Januari 17, 2006 (FH) - Shahidi wa upande wa utetezi katika kesi inayomkabili mkuu wa zamani wa mkoa wa Kigali Vijijini, François Karera, ameimbia Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kwamba polisi aliyekuwa akimlinda mkuu huyo alimuua kaka yake na wanaume wengine 18 wa kabila la Kitutsi Aprili, 1994. Shahidi huyo aliyetoa ushahidi kwa jina bandia la BMF kwa ajili ya usalama wake alikuwa ni jirani wa karibu sana na mtuhumiwa huyo.

10.01.06 - ICTR/KARERA - KESI YA MAUAJI YA KIMBARI DHIDI YA KARERA YAANZA KUSIKILIZWA

Arusha, Januari10, 2005 (FH) - Kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kigali Vijijini,nchini Rwanda, François Karera imeanza kusikilizwa rasmi mbele ya Mahakama ya Umoja wa Mataifa (ICTR) mjini hapa Jumatatu wiki hii. Karera ambaye alikuwa mtumishi wa siku nyingi serikalini anakabiliwa na mashtaka manne ya mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya binadamu aliodaiwa kufanya wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, mwaka 1994.

Dossiers