28.11.06 - ICTR/KARERA - MWENDESHA MASHTAKA AOMBA KIFUNGO CHA MAISHA KWA KARERA
Arusha, 27 Novemba 2006 (FH) – Mwendesha mashtaka katika Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji za Rwanda (ICTR) ameiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya maisha kwa François Karera kwa kesi ya mauaji yaliyofanyika mwaka1994.
Karera, mwenye umri wa miaka 67, alikuwa gavana wa Kigali vijijini .
Mwendesha mashtaka kutoka Rwanda Bi Florida Kabasinga alitoa ombi lake Alhamisi wiki iliopita mbele ya majaji wa mahakama mjini Arusha.
Aliambia mahakama kwamba mtuhumia alikuwa na uwezo wa kuzuia mauaji na kudumisha usalama katika vitongoji vya Kigali.
“Kutokana na uwezo aliokuwa nao serikalini, alikuwa na uwezo mkubwa kwa kuwalinda watu wake. Hivyo alikuwa anajua swala zima la ukatili uliofanyika katika vitongoji vya Nyamirambo, Ntarama na Rushashi alivyokua akiviongoza,” alisema
Kesi ya kiongozi huo ilifikishwa mahakamani Januari 9 mwaka huu.
Karera alikamatwa nchini Kenya mwaka 2001.
AS/AT


