US

09.04.08 - ICTR/US - BINGO YA DOLA 5,000 KUSAKA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA KIMBARI BADO IPO

Arusha, Aprili 9, 2008 (FH) – Balozi Maluum wa Marekani Anayeshughulikia Uhalifu wa Kivita, Clint Williamson amesititiza kwamba tuzo ya dola milioni tano (sawa na Sh bilioni zaidi ya tano) zilizotolewa na nchi yake kuwazawadia watakaotoa taarifa za kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa wa mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita ambao wako mafichoni, bado zipo palepale. Tuzo hiyo inayojulikana kama US Reward for Justice Programme inalenga kutoa motisha kwa watu wengi zaidi kushiriki katika juhudi za kuwasaka watuhumiwa maarufu wa mauaji ya kimbari na uhalifu wa kivita ambao hadi sasa bado wako mafichoni katika nchi mbalimbali.

Dossiers