Canada

17.04.08 - ICTR/CANADA - ICTR KUSIKILIZA OMBI LA WAZIRI ALIYEACHIWA HURU KUISHI CANADA

Arusha, Aprili 17, 2008 (FH) – Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Jaji Dennis Byron amekubali kusikiliza maombi ya Waziri wa zamani wa Usafirishaji na Mawasiliano wa Rwanda, Andre Ntagerura ya kutaka kwenda kuishi Canada baada ya kauchiwa huru kwa tuhuma za mauaji ya kimbari. Ntagerura Novemba mwaka jana aliiomba ICTR kuiamuru Canada kumpatia hifadhi ya kuishi nchini humo akidai kwamba nchi hiyo imekuwa ikipuuzia ombi hilo mfululizo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.

Dossiers