26.08.11 - ICTR/MAJAJI - ICTR YAPATA MAKAMU WA RAIS MPYA

Arusha, AGOSTI 26, 2011 (FH)-Jaji kutoka nchini Denmark, Vagn Joensen, amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari cha ICTR Alhamisi, Rais wa Mahakama hiyo Jaji Khalida Rachid Khan kutoka Pakistani, Agosti 24, 2011 alitangaza kuwa Makamu huyo mpya ataanza kazi zake rasmi Agosti 26, 2011.

Anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Jaji Dennis Byron (St. Kitts and Nevis), ambaye anarejea chini mwake kuwa Rais wa Mahakama ya Haki ya visiwa vya Caribiani. 

Jaji Joensen alijiunga na ICTR Mei 1997 na baadhi ya kesi anazosikiliza ni pamoja na ile ya kuhifadhi ushahidi inayomhusu anayedaiwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji ya kimbari anayesakwa vikali na mahakama hiyo, Felicien Kabuga.

Alizaliwa mwaka 1950 na ana shahada ya pili ya sheria ya Udhamivu na alikuwa akifundisha maswala ya kikatiba, jinai na madai katika Vitivo vya Sheria katika Vyuo Vikuu vya Aarhus na Copenhagen.

FK/NI

© Hirondelle News Agency