ICTR/Appeal

14.03.12 - ICTR/RUFAA - RUFAA YA KESI YA KANYARUKIGA KUTOLEWA HUKUMU MEI 8

Arusha, Machi 14, 2012 (FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) itatoa hukumu ya kesi ya rufaa ya mfanyabiashara wa zamani nchini Rwanda, Gasper Kanyarukiga, Mei 8, 2012.

21.10.10 - ICTR/RUFAA - WAKILI WA ICTR KUJIBU TUHUMA ZA KUKANA MAUAJI YA KIMBARI

Arusha, Oktoba 21, 2010 (FH) - Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Rwanda, Martin Ngoga amewaambia waandishi wa Habari Alhamisi kwamba nchi yake itamwita Wakili wa utetezi wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Peter Erlinder katika wiki chache zijazo ili kukabiliana na mashtaka ya kukana mauaji ya kimbari.

08.09.09 - ICTR/RUFAA - MAHAKAMA YA RUFAA YA ICTR KUSIKILIZA RUFAA TATU MWISHONI MWA MWEZI HUU

Arusha, 8 Septemba, 2009 (FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) mwishoni mwa mwezi huu itasikiliza rufaa za kesi tatu ikiwa ni pamoja na kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Protais Zigiranyirazo aliyekuwa shemeji yake Rais wa zamani wa Rwanda, marehemu Juvenal Habyarimana.

10.04.09 - ICTR/NGIRUMPATSE - ICTR YAAMURIWA KUFIKIRIA UPYA UAMUZI WAKE

Arusha, Aprili 10, 2009 (FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imefuta uamuzi wa awali wa ICTR wa kumnyima, mtuhumiwa Mathieu Ngirumpatse, Rais wa zamani wa chama tawala cha MRND nchini Rwanda kupewa ruhusa ya kutolewa kizuizini kwa muda ili kwenda kupata matibabu barani Ulaya. Jaji Kiongozi wa Mahakama hiyo ya Rufaa, Liu Daqun katika uamuzi wake uliotolewa Aprili 7, mjini The Hague, Uholanzi, aliamuru ICTR kufikiria upya uamuzi wake. ‘'Mahakama ya Rufaa inadhani kwamba ni muhimu kulirejesha suala hilo kwenye Mahakama inayoshughulikia kesi hiyo kutumia viwango vinavyotakiwa kisheria katika kutoa uamuzi wa suala hilo,'' alisisitiza Jaji, Daqun. Alifafanua kwamba, Mahakama yake imegundua kuwa mahakama ya awali inayoshughulikia kesi hiyo imefanya makosa katika kutumia madaraka juu ya uamuzi wa suala hilo. Ngirumpatse ambaye tangu Agosti mwaka jana hali ya afya yake imekuwa ikidorora aliomba kuhamishwa kutoka hospitali moja mjini Nairobi, Kenya anakotibiwa hivi sasa apelekwe Ulaya kwa matibabu zaidi. Katika uamuzi uliotolewa na ICTR na kutiwa saini na Rais wake, Jaji Dennis Byron, amefafanua kwamba mtuhumiwa anaweza kuhamishiwa sehemu nyingine kwa ajili ya matibabu lakini pia yalielezea mapungufu yaliyokuwemo ndani ya maombi wa kiongozi huyo wa MRND. Uamuzi wa Jaji Byron pia umezingatia ushauri wa kitaalamu uliotolewa na idara ya Tiba ya mahakama hiyo ambayo imeeleza kwamba mtuhumiwa huyo hivi sasa anapata matibabu bora kadiri inavyowezekana. Kufuatia hali ya kuugua kwa muda mrefu mtuhumiwa huyo, mahakama Machi 3, mwaka huu ilitoa amri ya kumwondoa mtuhumiwa huyo katika kesi ya pamoja na viongozi wenzake wawili wa chama hicho, aliyekuwa Makamu wa Rais wa MRND, Edouard Karemera na katibu wake Mkuu, Joseph Nzirorera. Lakini baadaye uamuzi huo pia ulitenguliwa baada ya Ngirumpatse kuruhusu wakili wake aendelea na kesi hata kama yeye hayupo mahakama. Kesi hiyo ya wanasiasa ilianza kusikilizwa Septemba 19, 2005 ambapo mwendesha mashtaka alihitimisha kesi yake Desemba 4, 2007 na Aprili 7, mwaka jana Karemera akawa mtuhumiwa wa kwanza kuanza kuleta mahakamani mashahidi wa kumtetea. Kesi hiyo iliahirishwa Aprili 1, kutokana na kukosekana kwa mashahidi na inatarajiwa kuendelea kusikilizwa Aprili 20 ambapo shahidi wa 32 wa utetezi wa mtuhumiwa Karemera atapanda kizimbani. Watuhumiwa wote walikana mashtaka ya mauaji ya kimbari na ukatili dhidi ya binadamu. SC/NI © Hirondelle News Agency

24.03.09 - ICTR/KABILIGI - HATAKATA RUFAA KUACHIWA HURU KWA AFISA MWANDAMIZI WA JESHI LA RWANDA

Arusha, Machi 24, 2009 (FH) - Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) amethibitisha kwamba hatakata rufaa dhidi ya kuachiwa huru kwa aliyekuwa Mkuu wa  Operesheni za Jeshi la Rwanda, Brigadia Jenerali Gratien Kabiligi, 58, Desemba 18, 2008.

02.02.09 - ICTR/KARERA - MAHAKAMA YATHIBITISHA KIFUNGO CHA MAISHA DHIDI YA MKUU WA MKOA

Arusha, 02 Februari , 2009 (FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu imethibitisha kifungo cha maisha jela kwa muda wote uliosalia wa maisha yake  mkuu wa zamani wa mkoa wa Kigali Vijijini, Froncois Karera baada ya kukubaliana na hukumu ya awali kuwa alihusika katika mauaji ya kimbari ya Rwanda mwaka 1994.

30.01.09 - ICTR/KARERA - RUFAA YA KESI YA MKUU WA ZAMANI WA MKOA KUTOLEWA JUMATATU IJAYO

Arusha, 30 Januari , 2009 (FH) - Mahakama ya Rufaa ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) Jumatatu ijayo itatoa hukumu ya kesi ya rufaa ya mkuu wa zamani wa mkoa wa Kigali Vijijini, Froncois Karera ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jela Desemba 7, 2007.

20.01.09 - ICTR/ZIGIRANYIRAZO - WAPINGA KIFUNGO CHA MIAKA 20 ALIYOPEWA SHEMEJI YA HABYARIMANA

Arusha, Januari 20, 2009 (FH) - Pande zote mbili za mashtaka na utetezi katika kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Protais Zigiranyirazo, 70, shemeji ya Rais wa zamani wa Rwanda, hayati Juvenal Habyarimana zimekata rufaa kupinga hukumu na adhabu aliyopewa mtuhumiwa huyo ya kifungo cha miaka 20 jela, Desemba mwaka jana.

14.01.09 - ICTR/BIKINDI - APINGA ADHABU YA KIFUNGO CHA MIAKA 15 ALICHOPEWA MWIMBAJI WA ZAMANI

Arusha, Januari 14, 2009 (FH) - Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Hassan Jallow amekata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 15 jela alichopewa msanii na mwimbaji wa zamani wa Rwanda, Simon Bikindi mwezi uliopita akidai kwamba mfungwa huyo anastahiki adhabu kali zaidi.

14.01.09 - ICTR/MILITARY I - MWENDESHA MASHTAKA AOMBA MUDA ZAIDI KUWASILISHA RUFANI YA KABILIGI

Arusha, Januari 14, 2009 (FH) - Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) anaomba muda wa kuwasilisha rufaa dhidi aliyekuwa  Mkuu wa Operesheni za Kijeshi wa Rwanda, Brigadia Jenerali, Gratien Kabiligi, 57, aliyeachiwa huru baada ya kufanikiwa kujitetea kwamba wakati wa mauaji hayo yeye alikuwa masomoni nje ya nchi.

Dossiers