Justice Info

Rwanda

16.10.12 - RWANDA/ICTR - RWANDA YAKANA KUKOSA FEDHA KUGHARIMIA KESI YA UWINKINDI

Arusha, Oktoba 16, 2012 (FH) – Rwanda, Jumanne imekanusha ripoti kwamba timu ya utetezi ya mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Mchungaji Jean Uwinkindi imekosa fedha za kuwawezesha kufanya upelelezi na kuwatafuta mashahidi wa kumtetea mteja wao.

05.10.12 - RWANDA/DRC - RAIS KAGAME ADAI ICC IMEAANZISHWA KWA AJILI YA WAAFRIKA

Arusha, Oktoba 05, 2012 (FH) – Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Alhamisi amedai kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) yenye mamlaka ya kuwashitaki watuhumiwa wa mauaji ya kimbari,uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ni fimbo ya kisiasa iliyoanzishwa kwa lengo la kuwapiga waafrika.

29.08.12 - RWANDA/JUSTICE - MAHAKAMA NCHINI RWANDA YAKATAA KUMWACHIA KWA DHAMANA UWINKINDI

Arusha, Agosti 29, 2012 (FH) – Mahakama mjini Kigali, Jumatano ilikataa ombi la kumwachia kwa dhamana mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Jean Uwinkindi kutokana na kilichoelezwa na mahakama hiyo kuwa ‘’uzito wa mashitaka anayokabiliwa nayo na wasiwasi kwamba huenda atatoroka.’’

13.08.12 - RWANDA/JUSTICE - MCHUNGAJI UWINKINDI AKATAA KUJIBU MASWALI YA MWENDESHA MASHITAKA

Arusha, Agosti 13, 2012 (FH) – Mshitakiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda, Jean Uwinkindi, amekataa kwa mara ya nne mfululizo kujibu maswali ya mwendesha mashitaka wa Mahakama Kuu ya Kigali, nchini Rwanda alikopelekwa kusikilizwa maelezo ya awali ya kesi inayomkabili.

06.08.12 - ICTR/USA - MAREKANI YAAHIDI ZAWADI ZAIDI KUWATIA MBARONI WASHITAKIWA WA MAUAJI YA KIMBARI

Arusha, Agosti 06, 2012 (FH) – Marekani imerudia msimamo wake wa kusaidia juhudi za kuwasaka watuhumiwa tisa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ambao bado hawajatiwa mbaroni na Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR).

28.03.12 - ICTR/CANADA - MTUHUMIWA WA CANADA AOMBA KUTUMIA KUMBUKUMBU ZA KESI 15 ZA ICTR

Arusha, Machi 28, 2012 (FH) – Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda anayekabiliwa na mashitaka hayo nchiniCanada, Jaques Mungwarere amerudia tena maombi yake ya kutaka aruhusiwe kutumia kumbukumbu za kesi 15  za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) ili kujenga utetezi wake.

10.11.11 - RWANDA/GACACA - MAHAKAMA ZA GACACA KUHITIMISHA KAZI ZAKE DESEMBA

Arusha, Novemba 10, 2011 (FH) - Wakuu nchini Rwanda wanasema Mahakama za Jadi zinazoshugulikia kesi za mauaji ya kimbari maarufu kama Gacaca zitahitimisha kazi zake ifikapo Desemba 31, mwaka huu licha ya kwamba kesi 22 bado hazijashughulikiwa.

02.06.10 - RWANDA/USA - ATAKA MMAREKANI ANAYESHIKILIWA RWANDA AACHIWE HURU MARA MOJA

Arusha Juni 02, 2010 (FH) - Wakili wa utetezi katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR), Vincent Courcelle-Labrousse Jumatatu wiki hii alitamka Mahakamani kuunga mkono juhudi zinazofanywa na mawakili wengine kumtoa nje mwanasheria wa Marekani aliyewekwa ndani nchini Rwanda kwa madai ya kukana kuwepo kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

23.04.10 - RWANDA/GENOCIDE - WATAHADHARISHA UFUNDISHAJI HISTORIA YA MAUAJI YA KIMBARI SHULENI

Kigali, Aprili 23, 2010 (FH) - Miaka 16 baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 yaliyoacha watu wapatao 800,000 wakiwa wamepoteza maisha, wengi wao wakiwa Watutsi na Wahutu wachache wenye msimamo wa wastani, Rwanda sasa inafikiria jinsi ya kufundisha somo la historia ya mauaji ya kimbari katika ngazi mbalimbali za elimu ikiwa ni pamoja na shule za msingi na sekondari. Tayari somo hilo linafundishwa kwa wanavunzi wa vyuo vikuu. 

16.04.09 - RWANDA/GENOCIDE - IBUKA YAZITAKA NCHI ZA MAGHARIBI KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHIMWA

Kigali, Aprili 16, 2009 (FH) - Chama cha Walionusurika na Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (IBUKA) kimesema kwamba nchi  za Magharibi zina jukumu la kusaidia kuwasaka na hatimaye kuwatia mbaroni watuhumiwa wa mauaji hayo ambao bado wapo mafichoni.