Fugitives
12.05.06 - RWANDA/FUGITIVES - JUMUI YA ULAYA YATAKIWA KUISAIDIA ICTR KUSAKA WAHALFU WA MAUAJI YA KIM
Arusha, Mei 11, 2006 (FH) - Serikali ya Rwanda imeitaka Jumuia ya Ulaya (EU) kuipa ushirikiano wa kutosha Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) kama inavyoiunga mkono Mahakama ya Kimataifa ya Wahalifu wa Kivita katika Yugoslavia ya zamani (ICTY) katika kuwasaka na kuwatia mbaroni watuhumiwa wa ICTR wanaoishi barani Ulaya. Mwakilishi wa Serikali ya Rwanda ICTR, Aloys Mutabingwa aliiambia Hirondelle kwamba EU ilionyesha nia thabiti katika kuwasaka wahalifu wa kivita na kuwatia mbaroni kama ilivyofanya kwa Kamanda wa zamani wa jeshi la Serbia, Ratko Mladic.
