13.08.07 - RWANDA/GENOCIDE/FILM - HAKUNA ANAYEWEZA KUUMIA KAMA MWATHIRIKA WA MAUAJI (KAGAME)

Kigali 10 Agosti 2007 (FH) - " Hakuna anayeweza kuumia kama mnusurika wa mauaji ya kimbali “alisema rais Paul Kagame kama ilivyonukuliwa na kituo cha redio ya Rwanda Ijuma iliyopita.

Rais Kagame aliyasema hayo Alhamisi wakati wa kufunga maonyesho ya filamu ilitumia kitabu cya aliyekuwa kamanda wa walinda amani nchini Rwanda kati ya Aprili na Julai mwaka 1994, jenerali Roméo Dallaire kutoka Canada.

"Hata kama kila mtu anajitahidi kuonyesha ni kiasi gani aliumizwa na matukio ya vita, lakini aliyeumia zaidi ni mwathirika wa mauaji ya kimbari “, alisema Kagame ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.

Roméo Dallaire alikuwa hana uwezo wa kuzuia mauaji ya kimbari yaliyochukuwa maisha ya watutsi na wahutu karibia milioni moja na vile vile hakuweza kuzuia kuuawa kwa walinda amani kumi wakiwa ni miongoni mwa wananakikosi alichokuwa akikiongoza Dallaire.

Ikiongozwa na wataalamu katika maswala ya kutengeneza filamu kutoka Canada, filamu hiyo ilitumia kitabu cha Dallaire kinachozungumzia matukio ya Rwanda kiitwacho ‘Nilishika viganja vya Ibilisi’, toleo la mwaka 2003.

Wazazi wa Mkurugenzi wa filamu hii, Laszlo Brana, ni waathirika wa mauaji ya kikatili ya mwaka 1945.

Katika mahojiano mwaka 2003, Dallaire, akiwa ameathiriwa na mauaji ya kimbari ya Rwanda alisema: "Moyo wangu unatangatanga katikati ya milima na roho yangu iko na watu waliouawa”

Filamu hiyo ambayo ilionyeshwa Rwanda, itaonyeshwa pia mjini Toronto ambako anaishi Dallaire kama seneti.

AS/AT