Justice Info

TPIR

I. Shughuli za mahakama

 

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za mauaji ya Rwanda, ICTR, imeanzishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mmataifa ,ONU, kwa mujibu wa maamuzi yake kifungo 955 ya Novemba 8, 1994. Ni mahakama ya pili iliyoanzishwa na ONU baada ya mahakama ya iliyokuwa Yougoslavia TPIY iliyoanzishwa mwaka 1993.

 

Vipindi vya Mahakama ya ICTRICTR ilipata uwezo wa kufuatilia washiriki wa mauaji ya kimbali pamoja na uvunjwaji wa haki ya kimataifa ya kibinadamu uliofanywa nchini Rwanda  na wananchi wengine wanaokisiwa kuwajibika na ukatili katika nchi jirani na Rwanda mwaka 1994.

 

Makao makuu ya ICTR yapo mjini Arusha nchini Tanzania na vile vile ina ofisi zake mjini Kigali nchini Rwanda zinazoshughulika hasa na utafiti, na ofisi zilizopo Haye nchini Uholanzi zinashughulikia kesi zilizopo mbele ya mahakama ya rufaa.

 

ICTR imeajiri watu 1000 kutoka nchi zaidi ya  80.

 

Mwishoni mwa mwaka 2007, itagharimu jamii ya kimataifa dola za kimarekani 1.032.692.2. Bajeti ya kwanza ya muhula wa mwaka 1994/1995 ilikuwa dola za kimarekani milioni 7.28 na kutarajia kufikia dola za kimarekani milioni 250 mwaka 2006/2007.

 

Gharama ya kesi iliyokadhiriwa na wengi kati ya mawakili wa utetezi ni dola za kimarekani 500.000 kwa mshtakiwa mmoja ndani ya wastani ya miaka miwili ya mwendelezo wa kesi moja.

 

ICTR ina idara tatu ikiwemo chemba ya mahakama ya rufaa, ofisi ya mwendesha mashtaka inayoshughulikia utafiti na ufuatiliaji, pamoja na ofisi ya msajili inayowajibika na utawala na kushughulikia chemba pamoja na pande zote.

 

ICTR ina chemba za mahakama ya mwanzo tatu zenye majaji wa kudumu 11, kati yao wawili wenye makao yao katika chemba za mahakama ya rufaa. Ogasti 2002, baraza la usalama la umoja wa mataifa liliamua kuunda timu ya majaji wa muda wapatao 18 kwa madhumuni ya kuharakisha kesi mbele ya mahakama ya ICTR. Mwishoni mwa mwezi Machi 2004, majaji watano walianza kazi. Majaji tisa wa muda wanngeweza kuwepo katika muda huo huo.

 

ICTR ilitengeneza kituo cha mahabusu mjini Arusha yenye seli 91za wafungwa.

 

Ukiacha nchi ya Mali, nchi zingine tano zilisaini makubaliano ya kuwapokea wahukumiwa katika mahabusu yao. Nchi hizo ni pamoja na Benin., Swaziland, France, Italy na Sweden.

 

 ICTR itafunga mwaka 2008 kesi za mahakama ya mwanzo na kesi za mahakama ya rufaa zitafungwa 2010. Kesi ambazo zitakuwa bado hazijakamilika zitahamishiwa katika mahakama ya Rwanda. ICTR imeanza kuandaa mazingira ya uhamisho huo.

 

II. Matokeo ya kesi zinazoshughulikiwa

 

Kesi ya kwanza inayomhusu aliyekuwa meya wa Taba, jimboni Gitarama Rwanda ya kati, Jean Paul Akayesu ilianza kusikilizwa Januari9, 1997. Hukumu ya kifungo cha maisha ilitolewa Octoba2, 1998 kutokana na kubainika kufanya mauaji ya kimbali, kuhamasisha moja kwa moja jamii kufanya mauaji pamoja na kosa la ubakaji kama kitendo cha mauaji.

 

Tokea ilipoanzishwa mwaka 1994 hadi Machi 2007, imekwisha hukumu watu 33, kati yao 5 wameachiwa huru, 28 walihukumiwa vifungo mbalimbali, 9 wanasubili kusikilizwa, na 18 walikuwa wametoroka.

 

Kati ya wahukumiwa, maarufu ni pamoja na aliyekuwa waziri mkuu Jean Kambanda, alibainika kufanya mauaji ya kimbali pamoja na meya Jean –Paul Akayesu, mtu wa kwanza aliyetuhumiwa kwa kosa la ubakaji likiwa kama kitendo cha mauaji. Wengine maarufu mbele ya mahakama ya rufaa ni pamoja na wana habari wakongwe watatu viongozi wa vyombo vya habari. Wanahabri hao ni pamoja na Ferdinand Nahimana, mhasishaji wa kituo cha redio televishen cha RTLM, Hassan Ngeze, mkurugenzi na mhariri mkuu wa jarida la Kangura pamoja na mkurugenzi wa maswala ya siasa katika wizara ya mambo ya nje na mwanakamati ya awali ya RTLM Jean- Bosco Barayagwiza amabye alihukumiwa kifungo cha miaka thelathini na mitano jela.

 

Upande wa wanaoshikiliwa na kituo ambao kesi zao zinaendelea mbele ya mahakama ya ICTR ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi wa baraza la mawaziri katika wizara ya ulinzi, kanali Theoneste Bagosora na Pauline Nyiramasuhuko akiwa mwanamke wa kwanza kushtakiwa kwa kosa la ubakaji kama kosa la jinai mbele ya mahakama ya kimataifa.

 

Wafungwa sita wanatumikia vifungo vyao nchini Mali. Wafungwa hao ni pamoja na waziri mkuu wa zamani Jean Kambanda, aliyekuwa gavana wa Kibuye Clément Kayishema, meya wa zamani wa jimbo la Taba, Jea-Paul Akayesu, mfanyabiashara Obed Ruzindana, mkurugenzi wa zamani wa kiwanda cha majani ya chai Gisovu wilayani Kibuye Alfred Musema pamoja na kiongozi wa jeshi katika jimbo la Gisenyi magharibi, Omar Serushago.

 

Mshtakiwa ambaye alikuwa askofu wa kanisa la anglicana la Shyogwe(jimboni Gitarama, Rwanda ya kati), Samuel Musabyimana alifariki akiwa bado ameshikiliwa Januari24, 2003.

 

Joseph Serugendo kiongozi wa zamani wa mitambo katika kituo cha RTLM alifariki Agosti22, 2006 katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya. Juni2, 2006, alihukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kukili kosa la kuhamasisha mauaji ya kimbali mwaka 1994.